Tayari headlines za majina ya waliopitishwa na Vyama Kugombea Urais zilichukua uzito sana kwenye stori kubwa Tanzania kwa muda mrefu, baada ya hatua hiyo sasahivi kinasubiriwa kuona Wagombea hao waliopitishwa kuanza kuchukua Fomu kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kwenye maelezo ya Jaji Damian Lubuva Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi “Tunaanza kutoa Fomu kwa wale wanaogombea urais, kesho UPDP watakuja kuchukua fomu saa tatu asubuhi wamesema hawana shamrashamra… TLP wao watakuja saa sita mchana wanakuja kwa shangwe… DP wao wanakuja saa nane mchana pia nao wamesema watakuja kwa shangwe pia”
“Jumanne August 4 watakuja CCM saa sita mchana watakuja kwa shangwe kama wengine… Jumatano watakuja ADC saa tatu asubuhi, wao hakuna shamrashamra baada ya hapo watakuja TADEA saa nne asubuhi pia wao hawana shangwe”
“August 17 watakuja ACT- Wazalendo saa tatu asubuhi wanakuja kwa shange pia… muda wa kuandisha wapigakura kwa mfumo wa BVR unaisha rasmi tarehe August 8 na baada ya hapo Ratiba ya Tume itaendeleakuruhusu Uchaguzi Mkuu” Jaji Damian Lubuva, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
0 comments :
Post a Comment