-->

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA JUMAMOSI 02.07.2017


Henrikh Mkhitaryan, 27, atakamilisha uhamisho kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United weekend hii. Mchezaji huyo kutoka Armenia atagharimu takriban pauni milioni 26 (Daily Mail), Manchester City wapo tayari kulipa hadi pauni milioni 50 kumsajili beki John Stones, 22, kabla ya kuanza kwa mechi za kabla ya msimu (Telegraph), Crystal Palace wamekubali kulipa pauni milioni 12.5 kumsajili beki wa West Ham James Tomkins, 27 (Daily Mail), mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanafikiria kumsajili beki wa kati wa Arsenal Laurent Koschielny, 30, ambaye mkataba wake Emirates unamalizika mwaka 2019 (Evening Standard), Everton wamekubali kumsajili kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel, 27, kutoka Zenith St Petersburg na watamlipa mchezaji huyo zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki (Squawka), Stoke City wametoa dau la pauni milioni 16 kutaka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, na wako tayari kumlipa pauni 70,000 kwa wiki (Mirror), Burnley wanataka kumfanya beki Michael Keane, 23, kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo ili kuzuia kusajiliwa na Leicester City (Mirror), mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie, 32, anauzwa na klabu yake ya Fernabahce (Evening Standard), mshambuliaji wa Manchester United Ashley Fletcher, 20, amekataa mkataba mpya na atafanya vipimo West Ham (Manchester Evening News). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Kumradhi sana, nilikuwa kimya kidogo kwa sababu niko safarini, nimefika Nairobi, naelekea Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment