Jua ndio kitu pekee ambacho kiko katikati ya mfumo wa jua. Jua ni 99.86% ya uzito(mass) wa mfumo wa jua.
Kimsingi jua ni mkusanyiko wa hydrogen na helium, 74.49% hydrogen na 23.8% helium.
Joto la kitovu cha jua linakadiriwa kufikia nyuzi joto milioni 15, wakati tabaka la nje lina nyuzi joto 5500.
Jua huchukua mwezi mmoja kumaliza mzunguko wake katika mhimili wake, na hii inakadiriwa tu na sababu kubwa umbo la jua ni kama mpira wa plasma. Kutokana na umbile lake, mzunguko hutofatiana tabaka na tabaka.
Mathalani, sehemu ya tabaka la nje karibu na ikweta yake, humaliza mzunguko wake kwa siku 25.4 wakati karibu na "poles" huchukua siku 36. Imethibitika tabaka la ndani la jua huzunguka kwa kasi zaidi kuliko tabaka la nje.
Wastani wa umbali kati ya jua na dunia ni km milioni 150 na mwanga husafiri kwa spidi ya km 300,000 kwa sekunde, teh, ukiwa mwanahisabati kama mimi na ukikokotoa utagundua mwanga wa jua hutumia dakika 8 kusafiri kutoka katika jua na kutufikia duniani.
Cha kufurahisha hapa, hii nishati hutumia dakika nane kutufikia duniani, lakini pia hutumia mamilioni ya miaka kusafiri kutoka katika kitovu cha jua na kufika katika tabaka la nje la jua(ambapo kutoka hapo ndio hutumia dakika 8 kufika duniani)
Hii ina maanisha nini? ina maanisha mwanga wa jua unao uona sasa si wasasa bali ulianza safari yake hadi kukufukia hapo ulipo mamilioni ya miaka.
Katikati ya kitovu cha jua asilimia kubwa ya nishati ya jua huzalishwa kutokana na mlipuko wa kinyuklia ambao huvunja(converts into) hydrogen kuwa helium. 99% ya nishati ya joto(thermal energy) inayotengenezwa na jua hutokea katika kitovu chake.
Wanasayansi wanasema kuwa jua iliundwa(formed) miaka bilioni 4.57 iliyopita kutokana kupasuka na kusambaratika kwa "giant molecular cloud" lilosheheni kwa wingi hydrogen na helium. Mpasuko huo ndio ukazaa nyota nyingi ikiwemo na nyota jua
Ikiwa sasa na umri wa miaka bilioni 4.5 jua iko nusu ya umri wake kama vile mtanzania akiwa na miaka 30 yuko nusu ya umri wake. Dunia imeshachoma nusu ya akiba yake ya hydrogen na kiasi kilichobaki kinakadiriwa kumalizika miaka bilioni 5 ijayo. Hydrogen kwa jua ni sasa na Petroli kwa gari.
Kwakuwa nyota jua iko katika jamii ya nyota zinazojulikana Yellow Dwarf, hivyo kuisha kwa hydrogen hakutasababisha kutokea kwa supernova(mlipuko mkubwa wa nyota), bali jua litabadilika na kuwa jekundu na kubwa zaidi kiasi cha kumeza sayari za karibu kama zebaki, zuhuru na dunia.
Kwa vyovyote vile hatutashuhudia kumezwa kwa kudunia, sababu kabla hata ya dunia kumezwa maji yote juu ya uso wa dunia na chini ta ardhi yatakuwa yanapotelea angani kama gesi, dunia haitakuwa na maji tena na joto lake litakuwa kubwa sana kiasi kila kiumbe hai afe. MWISHO WA DUNIA.
Hydrogen ikiisha na helium itaendelea kuchomeka kwa miaka milioni 130, kwa kupindi hicho jua na mfumo wa jua utakuwa umebadilika sana, na hilo likitokea orbiti ya dunia inakuwa si sehemu salama ya dunia.
Mambo yatakayo weza kufanyika ili kuwe na usalama ni kwa orbit hiyo kuahamishwa kabisa kutoka ilipo sasa, na kwakuwa jua litapoteza kabisa nishati yake ya sasa na kama tujuavyo uhai uliopo duniani unategemea sana nishati ya jua, hivyo salama zaidi ni kwa dunia na orbiti yake kuhamishwa kutoka katika mfumo wa jua na kwenda katika nyota nyingine ili mradi tu hiyo nyote iwe katika kundi la nyota za likenia katika galaxy ya milky way.
Ulimwenguni kuna mamilioni galaxy, inasemekana katika galaxy zote, ni galaxy ya milky way ndio kuna uhai(milky way is only known galaxy dat support life).
Wanaanga bado wanaendelea kuifanyia utafiti anga na ulimwengu kwa ujumla, tafiti zao huenda zitakuwa msingi mzuri kwa vizazi vijavyo kujua namna ya kuihamisha dunia au kugundua nyota nyingine yenye sayari inayoweza kuwa sawa na dunia hata watu wapate kuhamia huko pindi dunia ikifikia mwisho.
Wanasayansi wanakubali uwepo wa mwisho wa dunia na wanakubali kuwa nyota jua ina mwisho wake, lakini hakubali kuwa hayo yanasabishwa na mungu. Hata hivyo, wako busy kuhakikisha dunia haifikii mwisho.
Mbwana allyamtu
0 comments :
Post a Comment