-->

MAMBO 18 ALIYOFANYA JOHAN CRUYFF BARCELONA:-

1.Alitokea katika akademi ya Ajax na kununuliwa na Barcelona
2.wakati akiwa anaichezea Barca aliwahi kutishiwa na mfalme wa Hispania Dictator Franco kwamba ahame Barca na ajiunge na R.Madrid lakini alikataa.
3.Alisifika kwa style ya kuuzungusha mpira nyuma kwa mguu mmoja huku mwingine ukiwa mbele, style ambayo ilikuwa ngeni katika miaka ya 70 na inatumika mpaka sasa.
Zizou ameitumia sana.
4.Ndiye aliyeanzisha penati assist ambayo Messi aliipiga juzi pamoja na Suarez.
=kipindi Cruyff anaichezea Barca ndiye aliyeanza kuipiga akiwa na mchezaji mwenzake katika miaka ya 70.
Messi aliirudia juzi akiwa na Suarez ikiwa ni moja ya dedication ya kumuenzi Cruyff kutokana na taarifa zilizozagaa siku hiyo kuhusu tatizo lake la kansa.
5.Alishinda tuzo ya uchezaji bora wa dunia mara 3 mfululizo akiwa na Barcelona (balon d'or kwa sasa)
6.Baada ya kustaafu mpira akiwa kama mchezaji wa Barcelona alirudi kama kocha wa Barcelona
7.Ndiye aliyetoa wazo la kuanzishwa kwa chuo cha kukuza vipaji vya watoto wadogo (La Masia) ambapo wazo hilo aliiga toka akademi ya Ajax
8.Ndani ya muda mfupi tu Barca chini ya Cruyff iliweza zalisha vipaji vingi toka La Masia kama Eusebio Sacritus, Pep Guardiola, Andoni Zubizaretta, Angel Nadal na wengineo.
9.Cruyff ndiye mwanzilishi wa mpira wa tiki-taka.
10.Alichanganya staili ya mpira wa Uholanzi uitwao "total football" Uholanzi pamoja na staili yake na kuunda staili mpya ambayo inatumika mpaka sasa pale Barcelona "tiki taka"
ndiye baba wa tiki taka
11.Akiwa kocha mkuu wa Barcelona Johan Cruyff aliiwezesha klabu ya Barcelona kupata vikombe vingi kikiwemo kikombe cha kwanza cha Uefa iliyopata klabu hiyo mnamo mwaka 1992
12.kikosi cha Barcelona kilichokuwa chini ya Johan Cruyff kiliitwa "Barcelona The Dream Team" na kilitisha duniani kote.
13.Cruyff aliamua kuondoka Barcelona huku akiacha nembo yake katika klabu na historia kubwa ambayo haitakaa isahaulike.
14.Cruyff alipewa uraia na nchi ya Uhispania na kuwa na makazi maalumu katika jiji la katalan.
15.Cruyff amejenga academy mbili, moja iko Barcelona na nyingine ipo Uholanzi.
16.Cruyff alikuwa mshauri wa klabu ya Barcelona mpaka mauti yalipompata.
17.Amefariki kwa ugonjwa wa kansa.
18.Amefariki akiwa na miaka 68
🏼Barcelona ni cruyff na Cruyff ni Barcelona
Ulimwengu mzima wa soka unaomboleza kwa kifo cha Johan Cruyff..
*Football Legend
Para etern señor Johan Cruyff

Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment