Miguu kutoa harufu mbaya ni tatizo sugu linalowakabili baadhi ya watu katika jamii, wengi wakiwa wanaume. Tatizo hili linaonekana kuzidi kuwa sugu, hali inayosababisha kuwepo na harufu mbaya hasa kwenye mikusanyiko na wengi wao huwa wagumu kukubaliana na hali yao hata kutafuta tiba mahususi inaweza kuwaondolea kero hiyo.
Licha ya kuwepo sababu mbalimbali zinazochangia kutokea hali hiyo, ukweli utabaki kuwa uchafu ndio chanzo kikuu cha kuzaliwa kwa vijidudu vinavyoleta harufu mbaya kwenye miguu na kuwakera wanaokumbana na harufu hiyon.
TIBA YAKE.
Pamoja na tiba nyingine za kitaalamu ambazo mtu mwenye tatizo hili anaweza kupata, usafi ni jambo kubwa analopaswa kuzingatia zaidi. Ukigundua una tatizo hili, hakikisha unasafisha miguu, viatu na soksi zako mara kwa mara ili kuepusha unyevunyevu.Epuka kurudia soksi au kuvaa ambazo hazijakauka vyema kwani zinaweza kusababisha miguu kunuka mara dufu.Usivae viatu vilivyoloa na endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika kwenye hewa ili vikauke kupunguza uwezekano wa kutokea harufu.
Kama utahisi tatizo ni kubwa zaidi ni vyema utumie sabuni au poda zenye dawa za kuua vijidudu pamoja na mafuta maalumu yanayoweza kutumika miguuni.Unaweza kusugua miguu kwa kutumia chumvi, chokaa au kuvaa open shoes na sendo kuepuka tatizo ili.
Ikishindikana, nenda kwa wataalamu wa afya.
KWA HISANI YA Elizabeth Edward KUTOKA http://zanzibarelite.blogspot.com/
0 comments :
Post a Comment