SOMA DONDOO ZA BAJETI YA TAIFA 2013/14
1. Bajeti nzima ni Trilioni 18.2; ambapo Trilioni 11.1 sawa na 61% zitakusanywa kutoka kwenye mapato ya ndani (GBS itakuwa ni Trilioni 1.16, pia wafadhili watatoa Trilioni 2.7 ni misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo)
1. Bajeti nzima ni Trilioni 18.2; ambapo Trilioni 11.1 sawa na 61% zitakusanywa kutoka kwenye mapato ya ndani (GBS itakuwa ni Trilioni 1.16, pia wafadhili watatoa Trilioni 2.7 ni misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo)
2. Trilioni 5.7 zitatumika kwenye shughuli za maendeleo (ambapo Trilioni 2.7 zitatoka kwa wahisani; na Trilioni 3 zitatoka kwenye vyanzo vya ndani)
3. Matumizi ya kawaida ni Trilioni 12.5 (Trilioni 4.8 zitatumika kulipa mishahara na stahili za wafanyakazi; mfuko mkuu wa serikali umetengewa Trilioni 3.3 (kupunguza deni la Taifa) na matumizi mengineyo yatachukua Trilioni 4.5
4. Vipaumbele vya bajeti ni: Miundombinu, Kilimo, Viwanda, Rasilimali-watu, Utalii na Huduma za jamii
5. Deni la Taifa lafikia Trilioni 21
6. Kodi ya sigara, soda na bia imeongezeka kwa asilimia 10
7. Nia ya serikali ni kukuza pato la Taifa kufikia 7.2% mwakani (toka 7.0% mwaka huu); pia kudhibiti mfumuko wa bei toka 8.3% sasa na kufikia 6% mwakani
8. Kodi ya mishahara(PAYE) kupungua kwa asilimia 1; toka 14% na kuwa 13%
9. Kodi ya Mafunzo (Skill Development Levy) imepungua toka asilimia 6 mpaka 5
10. Watumiaji wa simu kutozwa 14.5% (ambapo asilimia 2.5 ya pesa hizo zitagharimia elimu)
11. Kutakuwepo na tozo mpya ya mafuta ya petrol y ash 50 kwa lita kugharimia umeme vijijini
12. 10% itatozwa kama kodi kwenye commission ya kusafirisha fedha kwa njia ya simu za mikononi
13. Ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi? KIMYA
14. Waziri hakuzungumza kuhusu bajeti ya elimu itakuwa kiasi gani (alijikita zaidi kwenye maeneo yaliyofanyiwa marekebisho baada ya bajeti za wizara mbalimbali kujadiliwa-la orodha ya vipaumbele aliyoitoa..hivyo-itakuwa inafanana na kiasi kilichopitishwa kwenye bajeti ya elimu cha shilingi bilioni 689.7 (bilioni 98.7 ni matumizi ya kawaida ya idara; bilioni 72.6 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo; na bilioni 518.4 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya taasisi (zikiwemo bilioni 306 za mikopo ya elimu ya juu).
SOURCE:LEWISMBONDE
0 comments :
Post a Comment