MAPROFESA na MADOKTA(PhD) WA TANZANIA NDIO CHANZO CHA UBOVU WA ELIMU YA TANZANIA. Kutokana na wanasiasa na wadau mbalimbali wa
elimu kumsakama Waziri Kawambwa na Baraza la mtihani la Taifa hii
inatokana na Viongozi wetu wa Tanzania kutokufanya tafiti ya kile
wanachokisema. Tanzania tuna Maprofesa na Madokta(PhD) wengi tu tena
wengine wa siku nyingi lakini hatuoni mchango wao katika kuboresha elimu
ya Tanzania zaidi wanaungana na wanasiasa kuendeleza porojo badala ya
kutoa ufumbuzi wa namna gani tutaiokoa elimu ya Tanzania.
Tulitegemea kuona Maprofesa na Madokta(PhD) kuibuka kwa nguvu kubwa
kuitaka serikali iunde mtaala wa elimu wenye tija kwa elimu ya
kitanzania na wao wakishiriki kutoa mchangoa wao badala yake ni
malumbano yasiyokuwa na tija. Hata tume inayotazamiwa kuundwa na waziri
mkuu tulitegemea Maprofesa wangekuwa wa kwanza kutoa ufumbuzi kabla hata
tume haijaanza kazi. Tunajua Maprofesa na Madokta(PhD) wanauwezo mzuri
wa kuandika mtaala wa elimu na sera nzuri ya elimu hata kutunga Vitabu
vizuri vya kufundishia kutokana na kiwango chao cha elimu lakini
tumewaachia Kina Nyambari watunge vitabu na watu wake wakati tuna wasomi
wa ngazi ya juu kabisa, tusiwe Taifa la kulaumu bali tuwe Taifa la
kujenga na kuona uchungu wa watoto wetu.
Hata kama tume ya waziri mkuu itapita bado suluhu haitapatikana kutokana
na wanao jua ukweli wamekaa kimya au kuamua kufanya kazi ya siasa.
Sambamba na mitaala na mfumo mbovu wa elimu wa nchi yetu bado serikali
inatakiwa kujitahimini juu ya mishara ya walimu kwani ni midogo sana na
haiendani kabisa na mazingira wanayoishi. Mwalimu mwenye degree analipwa
takribani 500,000/= na usheee, diploma takribani 300,000/= na ushee na
mwenyecheti takribani 200,000/= na ushee unategemea nini hapo?
Kimsingi mishara ni midogo sana na kila siku kodi za nyumba zinapanda
vyakula vinapanda, umeme unapanda kila mara nauli za daladala, kweli mtu
una weza kuishi? Huo huo mshahara ukatwe kodi ,ukatwe Nssf , ukatwe
CWT, chama cha kutetea haki za wafanya kazi wachukue chao.
1.Nauli kwa siku 800 kwa siku sita ni Tsh ngapi?
2.kodi ya chumba kwa mwezi 30,000/=
3.Chai asubuhi 800/=
4.chakula mchana 1200/=
5.kodi ya umeme 10,000/=
6.maji ya kununua ya madumu 300/=
7.Nyumbani uache 3500/=
8.Mtoto apate nauli ya shule na kula kwasiku 2000/=
9.Bado matumizi ya matibabu japo hili linatokea mara chache
Tunaomba mlitazame .
Lakini hutasikia wabunge na wanasiasa wanapiga kelele kutetea mishara ya
walimu ila wao kujiongezea posho wanajipigia kelele sana na wanaishi
maisha ya kifahari kuliko sisi walimu. Tulitegemea wabunge wange
wasilisha hoja binafsi ya kutetea mishahara ya watumishi ili wafanye
kazi kwa moyo wote lakini utafikiri hawaoni, daima tunajua mwenye shibe
hawezi kumkumbuka mwenye njaa. Mwalimu hata angejituma vipi kama
mshahara haukidhi ni vigumu kufundisha kwa kujituma maana lazima awaze
kufanya biasahara nje ya kazi ukizingatia mwalimu hana hata motisha.
Matokeo ya kidato cha nne yawe changamoto kwa serikali na si kutafuta
mchawi bali mchawi mkubwa ni mshahara mdogo na walimu kuthaminiwa.
Mwl.DEOGRATIUS KISANDU
Mwenyekiti wa JUKWAA LA WALIMU NA WANAFUNZI-TANZANIA.
25/02/2015
0 comments :
Post a Comment