Baada
ya kucheza England kwa miaka 11, mshambuliaji nyota wa Manchester
United, Robin van Persie anaachana na Premier League na kwenda kujiunga
na Fenerbahce ya Uturuki.
Mwenyekiti wa Fenerbahce Aziz
Yildirim amethibitisha kuwa mazungumzo ya uhamisho yamekamilika na Van
Perise anatarajiwa kutambulishwa rasmi Jumatatu kufuatia uhamisho wa ada
inayokaridiwa kufikiwa pauni milioni 3.4.
"Tumefanya
kazi kubwa hadi usiku wa manane. Tukapokea fax tano na sisi tukatuma
sita na hatimaye tukafikia muafaka (na Manchester United)," ananukuliwa Yildirim.
Kwa upande wake, Van Persie, Jumamosi alionekana akiagana na rafiki yake wa karibu Alderley Edge mmiliki wa mgahawa jijini Manchester.

Robin van Persie anakwenda kujiunga na Fenerbahce

Van Persie akisema kwaheri kwa swahiba wake Alderley Edge

Van Persie anakwenda kucheza nje ya England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11 ya kuitumikia Premier League

Van Persie akiagana na rafiki yake wa miaka mitatu katika jiji la Manchester
CREDIT: SALUTI 5.COM
0 comments :
Post a Comment