Imeripotiwa kwamba Messi alikua anatimiza ahadi yake ya kutembelea
Gabon kwa Rais Ali Bongo ambae anashutuma nyingi za udicteta na kula
rushwa. Bila kutegemea Messi akiwa na Deco walifika nchini Gabon na
Messi kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa uwanja wa Taifa wa Gabon.
Ripoti zilizotoka kwa wana habari wa ufaransa zinasema kwamba Messi
alipokea kiasi cha £2.4m ikiwa kama malipo yake ya kutembelea nchi hiyo.
Mwanzoni ziara hiyo ilipewa picha kama ni ya kujitolea kwenda kuzindua
uwanja wa taifa wa nchi hiyo. Wachambuzi
wa mambo wanasema kwamba kwa status ya Messi hata kama angepewa mualiko
na Rais huyo ingekua sio rahisi kwa yeye kukubali kwasababu Rais huyo
ana sifa mbaya ya kula rushwa. Pia ana kashfa ya kujilimbikizia mali
wakati wananchi wake wana hali mbaya na nchi yake ina watoto wengi
wanaoishi kwenye umaskini.
Wapinzani wa kisiasa wa Ali Bongo wanasema kwamba Rais huyo ametumia
pesa za walipa kodi kumlipa Messi ambaye anajihusisha sana na mambo ya
kujitolea duniani. Pia Ali Bongo inasemekana amemtumia Messi kwa ajili
ya kujipatia ushawishi zaidi kwa wananchi wake.
Messi
aliweka mikono yake kwenye cement mbichi ambapo mikono yake itabaki
kama kumbukumbu uwanjani hapo.Messi na Baba yake bado wana kesi ya
ukwepaji wa kodi nchini Hispania.
0 comments :
Post a Comment