Ikulu
ya White house imesema kuwa mipango ya kulifunga gereza la Guantanamo
Bay nchini Cuba imefikia awamu za mwisho. Rais Barack Obama anasemekana
kupatia kipa umbele suala la gereza hilo tangu aingie madarakani mwaka
wa 2009 lakini limekumbwa na vizuizi kadhaa.
gereza lililo n aulinzi mkali la Guantanamo
Gereza hilo la Guantanamo,
ambalo limepewa jina la umaarufu kuwa Gitmo - limekuwa likitumiwa na
Marekani kuwazuilia wapiganaji kutoka vita vya Iraq na vya Afghanistan
bila kufunguliwa mashtaka yoyote. Rais Obama alitoa agizo la kirais
kufungwa kwa kituo hicho mara moja katika siku yake ya kwanza. Lakini
baraza la Congress lilikataa kuwahamisha wafungwa wa huko kuwaleta
nchini Marekani kutokana na hofu za kiusalama.
gereza la Guantanamo
Baadhi ya wadadisi wanaamini
kuwa Marekani ilifungua gereza hilo nje ya ardhi ya Marekani ili
wanajeshi wake wapate fursa ya kutumia mbinu zilizopigwa marufuku katika
ardhi yao za kuwahoji wafungwa.
Gereza hilo pia limekumbwa kwa
miaka mingi na madai ya ukiukajji wa haki za binadamu, ambapo njia
zilizotumika kuwahoji wafungwa zimekashifiwa kuwa ukiukaji mkubwa wa
haki za binadamu. Aidha wafungwa wengi wamedai kuteswa, kupigwa na hata
kulazimishwa kukiri baadhi ya mashtaka.
wafungwa katika gereza la Guantanamo wamedai kuteswa
Wafungwa kadhaa maejaribu
kujitoa uhai kutokana na mateso wanayodai kupata huko. Wengine
wamechukua hatua kama kususia kula kwa wiki kadhaa kama njia ya
kulalamika hali duni ya kibinadamu katika gereza hilo.
wafungwa kadhaa wamerejeshwa makwao
Wengi tayari wamerejeshwa nchini mwao japo kunao baadhi ambao wanaaminiwa kuwa hatari zaidi na hivyo hawaja achiliwa.
Msemaji
mmoja wa ikulu ya white house ameambia waandishi kuwa mipango ya
kuwasafirisha wafungwa hao kwa njia salama imefikia awamu za mwisho na
itawasilishwa kwa baraza la Congress, lakini hakutoa maelezo zaidi.
0 comments :
Post a Comment