-->

BADO MASAA MACHACHE UKAWA KUVUNJIKA?

SHEREHE ZA KUVUNJA UKAWA???
Ndugu zangu,
Tangu jana nimeona MATAMKO ya watu mbalimbali wakijinasibu kwamba ni bora UKAWA ivunjike, wengine wanasema vyama vyao vinamezwa, wengine wanasema hawakubali hili na lile n.k. bahati mbaya haya yasemwayo ni mambo ambayo viongozi wa juu wa UKAWA ndiyo wanapaswa kuyashughulikia, si viongozi wa kawaida wa vyama au wanachama.
Mimi nataka tena kurudia kusema hapa, kwamba UKAWA ikivunjika kwa sababu yoyote ile, ni KITENDO CHA VYAMA VYA UPINZANI KUWASALITI WANANCHI. Hakuna lugha nyingine. Na wale wanaofurahia UKAWA ikitetereka na wanaoombea ivunjike waendelee kuomba maombi hayo yasiyo na tija kwa taifa.
UKAWA ikishavunjika vyama vya upinzani havitabaki salama hata kidogo. Athari ambazo chama kimojakimoja kinazipata ndani ya UKAWA ni chache kuliko chama kimojakimoja kikienda kivyake.
UKAWA ilikuwa na malengo makubwa sana, achilia mbali uchaguzi, kuna ajenda ya katiba. Tuliondoka kwenye bunge la katiba na kuacha milioni 30 kila mjumbe kwa sababu ya kujenga mshikamano wa upinzani. Kuvunja UKAWA leo ni kusema pia TUNAIKUBALI KATIBA inayopendekezwa.
Tukivunja UKAWA leo ‪#‎Tutapigwa_kwenye_uchaguzi_mkuu_huu‬ lakini zaidi ya yote ‪#‎Wananchi_Watatupiga_Mawe_Tutakapojipeleka_Kuwaambia_Waikatae_Katiba_Inayopendekezwa‬ kwani tutakuwa ‪#‎Hatuaminiki_Kwa_Mambo_Madogo_Na_Hatuwezi_Kuaminika_Kwa_Mambo_Makubwa‬.
Mimi naamini katika USHIRIKIANO WA VYAMA VYA KIMABADILIKO ili kulikomboa taifa, siamini kinyume chake hata kidogo. Kwa sababu viongozi waliahidi leo ndipo wataamua mustakabali wa kila kitu, kila mpenda mabadiliko anasubiri kwa hamu kujua viongozi wanaongoza tupite njia ipi.
Mungu awabariki nyote.
J. Mtatiro
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment