MAKUBWA!
Mchungaji wa Kanisa la Life in Christ Church Ministry maarufu kwa jina
la Kwajoe lililopo Tabata-Segerea, Dar, Prophet Joseph au Nabii Joseph
ameitwa polisi kisa kikidaiwa ni kuishi kinyemela na mke wa mtu
aliyetajwa kwa jina la Martha Raymond (32).
Kwa
mujibu wa chanzo makini, kabla ya ishu hiyo kufika katika Kituo cha
Polisi Tabata, Dar, mke huyo wa jamaa aitwaye Edward Kigoni ambaye pia
ni mama wa watoto watatu, aliondoka kwa mumewe tangu Agosti mwaka jana
hivyo katika kutafutwa ndipo ikabainika yupo kwa mchungaji huyo.
Ilidaiwa
kuwa baada ya kugundua hivyo, mara kadhaa ndugu wa Martha wamekuwa
wakifanya vikao kuhusu mgogoro kati ya wanandoa hao lakini Martha
amekuwa mgumu kurejea nyumbani kwake.
Ndugu
hao walidai kuwa kabla ya kugundua kuwa yupo kwa Nabii Joseph walikuwa
wakimtafuta kwa njia ya simu na kumtaka arudi nyumbani lakini alitoa
visingizio vya kuwa ‘bize’ na maombi, jambo lililosababisha kujitenga na
masuala ya kifamilia.
Akizungumza
na gazeti hili, Machi 2, mwaka huu, baba mzazi wa Martha, Mao Raymond
alidai hata yeye hajamtia machoni kwa zaidi ya miezi sita na mbaya zaidi
hakuhudhuria hata msiba wa dada yake uliotokea Desemba, mwaka jana
pamoja na kwamba alipewa taarifa kwa simu.
“Wakati tunamtafuta tuliambiwa anaishi kwa mchungaji huyo,” alisema baba huyo kwa masikitiko.
Machi 2, mwaka huu ndugu hao waliungana na kwenda kumchukua Martha kutoka katika kanisa hilo.
Hata hivyo, hawakufanikiwa kutokana na Martha kugeuka mbogo akikataa katakata na kurudi nyumbani huku akitoka mbio kukimbilia kanisani.
Machi 2, mwaka huu ndugu hao waliungana na kwenda kumchukua Martha kutoka katika kanisa hilo.
Hata hivyo, hawakufanikiwa kutokana na Martha kugeuka mbogo akikataa katakata na kurudi nyumbani huku akitoka mbio kukimbilia kanisani.
Kwa
kuheshimu kanisa, siku hiyo ndugu hao waliamua kumuacha kishingo upande
na kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Tabata, Dawati la Jinsia
ambapo mchungaji huyo alipelekewa barua ya wito ikimtaka ahudhurie kikao
kituoni hapo kuhusiana na sakata hilo la Martha lakini si yeye wala
Martha aliyehudhuria.
Waandishi
wetu walifuatilia sakata hilo hadi kanisani kwa Nabii Joseph ambaye
baada ya kuelezwa madai ya ndugu wa Martha, alikanusha taarifa za kuishi
na Martha.
Alipoulizwa kama anamfahamu Martha, alikiri kuwa anamfahamu kama mke wa mtu na muumini wake anayefanya shughuli zake kama kawaida.
Alipoulizwa kama anamfahamu Martha, alikiri kuwa anamfahamu kama mke wa mtu na muumini wake anayefanya shughuli zake kama kawaida.
Nabii
huyo alipoulizwa kama alipata barua ya wito kutoka polisi, alikiri
kupokea na kusema kuwa mara baada ya kupata wito huo, alimuita Martha na
kumshauri aende kituoni kukutana na mkuu wa kituo ili amuelezee kila
kitu.
Alidai
kuwa Martha alifanya kama alivyomshauri hivyo hakukuwa na sababu ya
yeye kwenda kituoni kwa shauri hilo, taarifa ambazo zilikanushwa kituoni
kwamba hawakufika wote.
Kwa
mujibu wa mume wa Martha, Kigoni yeye anachotaka ni mkewe kurudi
nyumbani huku akidai kuwa kwa upande wake unatimia mwaka sasa hajaonana
na mkewe zaidi ya kusikia kuwa yupo kwa Nabii Joseph.
Mke wa mtu.
“Ameondoka
na kuniachia watoto watatu. Nashukuru tu kwamba kwa sasa wapo shule za
bweni ila wakirudi likizo huwa napata shida sana kila siku wanamuulizia
mama yao na mara nyingine wanamfuata hadi huko kanisani kwake,” alisema
Edward.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
0 comments :
Post a Comment