Kikosi cha Barcelona kilichoanza.
FC Barcelona vs Manchester City, Mtanange wa kipindi cha kwanza unamalizika wa dakika 45 wakiwa bado 0-0, Hakuna cha Barca wa City, Barcelona wakijaribu mara kwa mara kuingia kwenye eneo la hatari la City bila kufunga, Neymar na Messi wakikosa mabao.
Wao
City nao wamejaribu kuingia lakini shuti lililopigwa na Nasri lilidakwa
na Kipa wa Barca. Kumbuka katika Mtanange wa kwanza walitoka 2-0 huko
Etihad na sasa Man City wanataka kupindua kipigo hicho cha bao hizo
mbili na kuwatupa nje Barcelona kwenye uwanja wao Nou Camp.
Messi na Aguero wakioneshana ubabe!
Kipindi cha pili dakika ya 67 Lionel Messi akaipachikia bao Barca baada ya mabeki wa City kujichanganya. Lescott akituliza mpira bila umakini na hatimae Messi kuuchukua na kutupia nyavuni. Dakika ya 78 Mchezaji wa City Pablo Zabaleta anaonshwa kadi ya njano na nyekundu na kutolewa nje ya uwanja baada ya kufanya ndivyo sivyo na Mwamuzi S. Lannoy kumtoa nje. Dakika ya 80 Barca walifanya mabadiliko Neymar alitoka na nafasi yake ilichukuliwa na Alexis Sánchez. Dakika za lala salama dakika ya 89 kona ilipigwa na hatimae Vincent Kompany akasawazisha bao kwa kufanya 1-1(Agg.3-1) na hapo hapo kwenye dakika za majeruhi dakika za nyongeza Barcelona walifanya mashambulizi na kupachika bao la pili kwa kufanya 2-1 (Agg. 4-1) Bao lililofungwa na Daniel Alves akipewa pasi safi na Andrés Iniesta Luján ndani ya box na kuachia shuti kali hadi ndani ya lango la City na mpira kumalizika. Ushindi huu wa Barca unawaondosha City nje ya michuano hii ya Uefa kwenye hatua ya 16 bora, Huku Barca wakisonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.
Kocha wa City kautazamia kwa mashabiki
Yaya Toure na pique wakichuana vikali
Silva akiupoza mpira
Iniesta mbele ya Vicent Kompany
Hapa hukatizi ndugu yangu ....hapa ni Nou Camp!
Chupu chupu hapa Vicent Kompany kidogo awapige bao la kichwa..katika kipindi cha kwanza.
Kidogo!!
Lescott akipitwa na Lionel Messi
Neymar baada ya kukosa bao la wazi hapa!!
Neymar akionekana kuumia kukosa bao!
Mtu kati...
Daniel Alves akichuana hapa ...nivute ni kuvute na David Silva
Neymar akiendesha...
Utakubali tuu!
Messi na Lescott
Picha mbali .....kaa pembeni!!
Nani fundi hapa!
Neymar kwenye patashika na wachezaji wa City!
Hoi!!! msaidizi wa kocha wa City Ruben Cousillas
Unakosa!!tutajutia baadae......
Benchi halikukalika!!!VIKOSI:
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Mascherano, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Messi, Fabregas, Neymar.
Subs: Pinto, Pedro, Alexis, Bartra, Song, Adriano, Sergi Roberto.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Kolarov, Silva, Fernandinho, Milner, Nasri, Toure, Aguero.
Subs: Pantilimon, Negredo, Dzeko, Javi Garcia, Jesus Navas, Clichy, Boyata.
Referee: Stephane Lannoy (France)
0 comments :
Post a Comment