picha
ikionyesha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM, wakila kiapo,
katikati ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA kata ya Orturumenti
Thomasi Kivuyo.
Mwenyekiti
wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkono kwa katibu wa
siasa uenezi Jonasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm
katibu wa vijana wilaya ya arumeru akiwa Boniface Mungaya akionyesha baadhi ya kadi zilizorudishwa na wanachama wa chadema.
Jumla
ya wananchi 100 wa kata ya Ortumunti wilayani Arumeru kutoka katika
vyama mbalimbali vya upinzani wamehamia chama cha Mapinduzi akiwemo
mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA wa kata hiyo .
tukio
hilo limetokea mwishoni mwa wiki,wakati wa mkutano wa hadhara wa
CCM,uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumeru
mkoani hapa.
Akiongea
wakati wa kurudisha kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya
CCM,Mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA, Thomasi Molel alisema kuwa
ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kubaini kuwa tangu awe mfuasi
wa cha hicho (CHADEMA),Hajapata faida yoyote wala hajaona kitu ambacho
wananchi wanafaidika kupitia chama hicho.
Alisema
kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia katika siasa tangu
mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo, hivyo ameamua kuondoka katika chama
hicho kwani CHADEMA ni chama ambacho hakina demokrasia ya kweli
ambayo inatakiwa iwenacho kama chama
Alisema
kuwa viongozi wengi wa CHADEMA wamekuwa wanatoa ahadi za uongo kwa
wananchi na mbali ya hivyo pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi
kwani kila kiongozi amekuwa anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji
mmoja ambaye ndie atakaeweza kukisemea chama .
Aidha
alibainisha kuwa katika kata yao tangu upinzani wameingia madarakani
hamna kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa
wakiwachangisha wananchi hela nyingi bila kufanya maendeleo yeyote
akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa kwa
kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana ela hiyo ingeweza kujengea
shule lakini adi leo hela hile aijafanya chochote na aijulikani
ilipopelekwa
Aliongeza
kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato na matumizi ya kata
yao tofauti na kipindi ambacho ccm ilikuwa madarakani hivyo.
Kwa
upande wake katibu wa ccm wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema
kuwa wao kama ccm wanawaapokea wananchama hao na pia wamesikia baadhi
ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na matumizi kwa
kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda katika
ofisi ya mkurugenzi kufuatilia swala hili.
Aliwasihi
wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi kunakoelekea uchaguzi
mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya kosa kwa
kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka na kata yao haitapata
viongozi wazuri.
0 comments :
Post a Comment