-->

MCHEZAJI MPYA WA MANCHESTER UNITED AWEKA REKODI AMBAYO RONALDO HAKUWAI KUIWEKA

Mchezaji mpya wa Manchester United, Anthony Martial baada ya jana usiku kufunga goli dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika michuano ya klabu bingwa Ulaya, ameweka rekodi ambayo ilimshinda Cristiano Ronaldo akiwa Old Trafford.



Akiwa na miaka 19 Martial ameshafunga magoli 5 katika mechi 9, huku katika umri huo huo Cristiano Ronaldo ilimchukua mechi 39 kufunga magoli hayo 5.



Kijana huyo raia wa Ufaransa amekuwa na mwanzo mzuri huku akimudu pressure iliyopo Old Trafford sanjari na dau kubwa sana alilosajiliwa akitokea Monaco ya Ufaransa.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment