Marcos
Rojo (mwenye T-shirt) akiwa na wafanyakazi wa Man Utd katika hospitali
ya Bridgewater ametua kukamilisha usajili siku ya leo kuchukuliwa
vipimo.
Mchezaji wa Argentina, Marcos Rojo.
Mshambuliaji wa Man Utd, Luis Nani amejiunga na Spoting Lisbon kwa mkopo.
KLABU ya Manchester United imekubali kutoa Pauni Milioni 16 kumnunua beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo.
Rojo, ambaye ametua mjini Manchester leo na kusema kuhamia United
‘anahisi kama ndoto’, anatarajiwa kusaini Mkataba wa miaka minne
akifaulu vipimo vya afya na kukubali vipengele binafsi vya kandarasi
yake.
Louis van Gaal ametoa kipaumbele kwa usajili wa beki huyo mtumia
mguu wa kushoto, Rojo, mwenye umri wa miaka 24, kufuatia kufungwa mabao
2-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England Jumamois na Swansea.
Winga
Luis Nani, aliyejiunga na United kutoka Sporting kwa Pauni Milioni 17
mwaka 2007, amerejeshwa kwa mkopo klabu yake hiyo ya zamani, ilia ni
sehemu ya dili hilo la Rojo.
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment