
KAMBI
ya Simba iliyopo mjini Lushoto, imetengemaa baada ya ‘bundi’ (balaa)
lililokuwa likiwaandama wachezaji wake kwa kukumbwa na majeruhi
kuyeyuka.
Wakati
kikosi cha Simba kikizidi kujifua vilivyo kujiandaa na msimu ujao wa
Ligi Kuu Tanzania Bara chini ya Kocha Mkuu Mwingereza, Dylan Kerr, kambi
hiyo ilianza kuingia doa kwa nyota kadhaa kukumbwa na majeruhi.
Wachezaji
hao ni Ivo Mapunda na Mussa Hassan ‘Mgosi’ ambao kwa sasa wapo fiti na
tayari wanaendelea na programu ya mazoezi ya Kerr na wasaidizi wake.
Kwa
mujibu wa daktari wa Simba, Yassin Gembe, Ivo na Mgosi wapo imara ikiwa
ni baada ya Ijumaa iliyopita kushindwa kufanya mazoezi ya pamoja na
wenzao kutokana na kusumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya, ikiwemo
majeraha hivyo kulazimika kupumzika.
0 comments :
Post a Comment