-->

MKULIMA ALIYECHUKUA FOMU YA URAISI NAYE AFUNGUKA YAKE YA MOYONI


Edelphonce Bilohe ‘Mkulima’
Edelphonce Bilohe ‘Mkulima’
Mmoja wa watia nia aliyechukua fomu kuwania kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang'anyiro cha Urais wa Tanzania 2015, Edelphonce Bilohe maarufu kama ‘Mkulima’ amenukuliwa na gazeti la MWANANCHI akilalamika na kusema kuwa hajaelewa mchakato mzima wa kuteua majina matano ulivyokwenda zaidi ya kushuhudia purukushani mjini Dodoma. 
Pamoja na kutoelewa mchakato wa uteuzi huo, Bilohe alilalamika kuwa tangu amefika Dodoma hajapata mapokezi mazuri kutoka kwa wana CCM wenzake au hata wale watia nia 38 waliobahatika kurudisha fomu. 
“Kila ninapojaribu kuuliza hiki au kile sipewi majibu, nimekaa hapa na wanaCCM wa mkoani, sijaonana na Nape (Nnauye) wala (Abdulrahman) Kinana, wala watia nia wenzangu” 

Alisema anashangaa kuwa hajahojiwa kama utaratibu wa uteuzi huo unavyotakiwa badala yake ameshindwa hata kujua wanaCCM wenzake walipo na wanafanya nini kwa wakati huo.
“Kuna makundi hapa, hali si nzuri, mpaka sasa sijaelezwa utaratibu wa mkutano wa halmashauri unavyokwenda. Nimezunguka nchi nzima, nitawaambia nini Watanzania. Hali ya hapa imeharibika” 
Bilohe alisema hajaridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea na alieleza kufurahishwa kwake na hatua ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa kuyapinga.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment