HABARI 4U MOVEMENT TANZANIA.
Tunayo
furaha kuwapongeza kwa uvumilivu na UMOJA wetu tulio uonesha na
tulionao hata sasa na kwa kipindi chote katika kumpambania Edward
Lowassa Kupata tiketi ya Urais ndani ya chama cha mapinduzi. Malengo
yetu Balozi wetu Edward Lowassa awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na si Ukatibu au Uenyekiti wa chama kwani Malengo yetu ni
ukombozi wa Maisha ya Watanzania wote. Tumesikitishwa
na vikao vya Maamuzi ya Chama kwa kuto Mpitisha mtu anae kubalika nje
na ndani ya chama kama alivyo sema Mwl. Julius Nyerere, 4u movement
haiungi Mkono maamuzi hayo yaliogubikwa na Sintofahamu nyingi. Tunawaomba
muwe watulivu na wenye subira kwani Mchakato wa Kidemokrasia wa kumpata
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado upo wazi kwa majibu Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumaini letu ni Lowassa kwa sababu ndie Pekee tunaemuamini na Anauwezo. Alipo Edward Lowassa Tupo. Pia
zipo Taarifa kuwa hayuko salama, hizo Taarifa si za kweli ni
upotoshaji. Edward Lowassa yupo salama na anaendelea na majukumu yake.
Tusubiri mpaka atakapo toa neno na sisi viongozi tutawajuza nini cha
kufanya. Tutawapatia muongozo kila inavyo bidi. Ahsanteni
Mr Hemed Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO
IMEWEKWA MTANDAONI NA: Gabriel Gregory Ishole

Mr Hemed Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO
IMEWEKWA MTANDAONI NA: Gabriel Gregory Ishole
0 comments :
Post a Comment