-->

MAJOKA YAPAKIWA KWENYE NDEGE ILI KWENDA KUUZWA ULAYA

Inasemekana ndege moja ya abilia ilikua imepakia abilia wapatao 240 na mizigo, lakini katika baadhi ya mizigo ndege iliyokua imepakia kukawa na nyoka wapatao 2000 waliokua wakisafirishwa kutoka Harare zimbambwe kwenda ulaya kwaajili ya kutumika kutengeneza bidhaa kama mikanda na mikoba ya akina mama
Lakini wakati wa kupakia mizigo ile wale nyoka hawakufungiwa vizuri, na ndege ilipofika juu wale nyoka wakaanza kutoka ili kutafuta hewa( Kadiri unavyopanda kwenda juu mgandamizo unaongezeka na oksijeni inapungua)

Wale nyoka wakafanikiwa kufika mpaka sehemu ya abilia, abilia walipowaona wale nyoka wengi wakaanza kupiga kelele na kuhangaika, ndipo rubani wa ile ndege alipokuja kuangalia nini kinaendelea, alipoaangalia akawaona wale nyoka wametoka na wamewazunguka baadhi ya abilia.
Yule mwongoza ndege akamwambia hutakiwi kutua chini, unachotakiwa kufanya ni kwenda juu zaidi, kwasababu wale nyoka wametoka chini kwenye mizigo kuja kwa abiria kutafuta oksijeni rubani alifanya hivyo na akafanikiwa kuwaokoa watu wote.
CHANZO:HABARI MPASUKO
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment