
Katika
mchezo huo ulioisha hivi punde mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji
Didier Kavumbagu katika sekunde ya 40 ya mchezo, kabla ya Msuva kufunga
bao la pili katika dakika ya pili.
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Uganda aliyeanza kuichezea Yanga leo tangu apewe ruhusa
na Fifa, Emmanuel Okwi akaziona nyavu za Ruvu katika dakika ya 27,
dakika 3 baadae Mrisho Ngassa akaipatia Yanga bao la 4. Hadi timu
zinaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Kipindi
cha pili Yanga wakarudi kwa kasi na kufanikiwa kuongezea mabao mawili
yaliyofungwa na Kavumbagu tena, Hamisi Kiiza na Saimon Msuva akafunga
hesabu kuhitimisha ushindi wa mabao 7-0.
0 comments :
Post a Comment