-->

HABARI YA KUSHANGAZA,MTAWA AJIFUNGUA PASINA KUJUA ALIYEMPA UJAUZITO


Mtawa wa kanisa Katoliki la Italia ambaye alikimbizwa hospitalini baada ya kulalamika kupata maumivu ya ghafla  ya tumbo amezaa mtoto wa kiume  aliyepewa jina la francesco (Francis).

Amejifungua mtoto mwenye kilo 3.5 (tatu na nusu) katika hospitali ya St. Camillus de Lellis, iliyoko katika mji wa Rieti, ulioko mkoa wa Lazio siku ya Jumanne ya tarehe 14, januari 2014.

Mtawa huyo mwenye umri wa miaka 31 na ambaye jina lake limefichwa ametajwa kama mtu aliyelitia aibu kanisa katoliki nchini Italia. 

Askofu wa eneo hilo la kaskazini ya Roma alisema kuwa Mtawa huyo hana budi kuondoka kwa kuwa amevunja nadhiri yake ya usafi wa moyo.


"Itakuwa vyema kwa yeye sasa kuishi maisha ya kidunia na mtoto wake na awe mbali na taasisi za kidini", alisema msemaji wa delio Lucarelli ambaye ni askofu wa Rieti.

Mtawa huyo kutoka nchi ya El Salvador alifanya siri kubwa juu ya ujauzito wake hata wakati anapelekwa hospitalini alikanusha kuwa anaweza kuwa na mimba. "Haiwezekani mimi ni mtawa", aliwaambia madaktari kwa mujibu wa shirika la habari la Italia la ANSA .

"Sikujua kama nilikuwa mjamzito, mimi nilihisi ni maumivu ya tumbo tu", alinukuliwa Mtawa huyo akiwaambia Madaktari.  
Alisisitiza kusema kuwa hajui mimba hiyo ameipataje kauli iliyowaacha wengi midomo wazi, na wengine kukaa kimya kushindwa kutoa neno lolote.

Inaelezwa kuwa huenda ujauzito huo ameupata wakati wa ziara ya nchini kwao mwaka jana. Dayosisi ya ndani ilisema Mtawa huyo na mtoto wake watapewa msaada kwa muda wa wiki chache mpaka itakapoamuliwa juu ya mustakabali wa maisha yake . 

Hali ya afya ya mama na mtoto imetajwa kuwa ni nzuri. "Wote mama na mtoto wapo katika afya njema ," alisema Pasquale Carducci , mkurugenzi wa hospitali za mitaa. 

Akizungumzia tukio hilo kwa niaba ya Masista wa kanisa, Sista Erminia alisema jambo hilo limewashangaza sana na kuwastua. "Inaonekana yeye hakuwa na uwezo wa kupinga majaribu", alisema sista Erminia.

Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment