-->

YAJUE MADHARA YA KUONGEA NA SIMU KWA MUDA MREFU,SHUHUDIA LIVE KATIKA PICHA

Karibu katika benchi la Teknolojia la BUSTANI YA HABARI. Leo tutaangalia jambo la ajabu kidogo na kama unabisha utajaribu mwenyewe kisha utajionea.
Matumizi ya Simu za kiganjani yameongezeka sana ndani na nje ya nchi. Simu hizi licha ya kuwa na msaada mkubwa katika maendeleo ya jamii pia zina mambo yake ambayo yanashangaza na kutisha kidogo/sana!!!!
Leo nitawaelekeza namna ya kupika yai kwa kutumia simu mbili za mkononi. Baada ya somo hili jaribu kufanya jaribio na ujionee mwenyewe.
Mahitaji: Simu mbili za kiganjani, Glasi/Bilauri ya maji na Yai ambalo halijapikwa wala kuvunjika.
Hatua: Chukua simu ya kwanza na upige kwenda namba ya simu yapili, pokea simu ya pili na kuiacha hewani kisha chukua glasi yenye yai na uiweke kati ya simu hizo mbili kwa dakika 65, ni vema ukajiunga na vifurushi ili usiingie gharama kubwa. Angalia mfano katika picha hii hapa chini. 

Baada ya dakika 65 yai litakuwa limeiva kabisa kama limechemshwa vile, Sikushauri ule yai hilo kwakuwa sijafanya utafiti wa kutosha endapo kuna madhara yoyote mtu akila au la.
Sasa chakujiuliza hapo ndugu zangu ni je, endapo mionzi hii ya simu inaweza kuivisha protein iliyopo katika yai vipi kuhusu ubongo wako, hasa kwa wale watumiaji wakubwa wa simu!!
source:KIJIWE CHA WASOMI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment