
Anelka, mwenye umri wa miaka 34, ameshutumiwa vikali kwa kufanya ishara hiyo, ambayo ilipigiwa debe sana na msanii wa Ufaransa Diedonne M'bala M'bala, ishara ambayo ilitajwa na wakosoaji kuwa ishara ya utawala wa Kinazi.
Mshambuliaji huyo wa Westbrom, amesema atapinga mashtaka hayo yaliyowasilishwa na Shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza.
Ikiwa atapatikana na hatia Anelka huenda akakabidhiwa adhabu ya kutoshirika katika mechi tano mfululizo.
Klabu ya Westbrom halijasema lolote kuhusiana na mashtaka hayo ya FA, lakini imekariri kuwa Anelka ataendelea kuichezea klabu hiyo hadi kesi hiyo itakapoamuliwa
CHANZO:BBC SWAHILI
0 comments :
Post a Comment