
Mbali na Rais Jakaya Kikwete, marais wa Uganda na visiwa vya Comoro nao wamehudhuria sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani kisiwani Unguja. Wengine waliohudhuria sherehe hizo ni maseneta kutoka miji ya Lamu na Mombasa Kenya, pamoja na mwakilishi maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China. Akihutubia sherehe hizo, Rais Ali Muhammed Shein wa Zanzibar amewataka wananchi waonyeshe umoja na mshikamano katika sherehe hizo.
Huku hayo yakiripotiwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, kuwa Siku ya Mapumziko kwa Watanzania wote ikiwa ni kufidia siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoangukia leo Jumapili. Tangazo hilo limekuja kufuatia tangazo kama hilo lililotolewa na Rais wa Zanzibar kwa wakazi wa visiwa vya Unguja na Pemba.
CHANZO:RADIO IRANI SWAHILI
0 comments :
Post a Comment