-->

HUYU NDIE MCHEZAJI MWENYE ELIMU KUBWA KATIKA LIGI KUU BARA

Lusajo anakuwa mchezaji raia wa Tanzania, mwenye elimu zaidi ya wachezaji wote wanaocheza Ligi Kuu kwa sasa ingawa anazidiwa kidogo na kipa wa Toto Africa, Erick Ngwegwe ambayo iko Ligi Daraja la Kwanza. STRAIKA wa Yanga, Reliants Lusajo ndiye mchezaji msomi kuliko wote ndani ya kikosi hicho lakini amekiri kwamba ana changamoto kubwa ya kupata namba ya kudumu. Lusajo amemaliza masomo yake ya Shahada (digrii) katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kilichopo mkoani Kilimanjaro alikokuwa akisoma Shahada ya Ugavi (Bachelor of Arts in Procurement). Mchezaji huyo amekosa michezo 10 ya ligi msimu huu kwa kuwa alikuwa akimalizia ripoti yake ya Utafiti (Research) kama sehemu ya masomo yake na mwezi ujao atatunukiwa shahada yake ya kwanza kwenye mahafali ya chuo hicho. Lusajo anakuwa mchezaji raia wa Tanzania, mwenye elimu zaidi ya wachezaji wote wanaocheza Ligi Kuu kwa sasa ingawa anazidiwa kidogo na kipa wa Toto Africa, Erick Ngwegwe ambayo iko Ligi Daraja la Kwanza. Uchunguzi wa Mwanaspoti umebaini kwamba wachezaji wengi wa klabu za Ligi Kuu wameishia darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na wachache wana elimu ya cheti. “Nlifurahi kucheza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu baina ya Yanga na Mgambo JKT, ligi ni ngumu na inahitaji mtu kufanya kazi kwa juhudi kubwa. “Yanga ina wachezaji wazuri na wenye uzoefu mzuri, nafikiri kwa kwa sasa nimemaliza masomo yangu hivyo nitahakikisha nafanya kazi yangu ya mpira kwa kujituma,” alisema Lusajo.
CHANZO:~MWANASPOTI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment