Niliwahi
kuuliza kwa watu wa nguvu shilingi milioni 75 wakipata watatumia kwenye
nini?, majibu ya wengi yalikua ni kujenga nyumba na kununua gari huku
wengine wakisema watawekeza kwenye biashara.Sasa basi, pamoja na hiyo milioni 75 kuonekana inaweza kufikiriwa kufanya mambo hayo makubwa ya kimaisha… imefahamika kiwango hicho cha pesa kinaweza kuishia kwenye kununua TV moja tu hii mpya ya Samsung ya inch 85 na usirudishiwe chenchi.
millardayo.com ilipotembelea duka lao Mlimani City, imeambiwa TV hii ina vitu vingi vya kipekee ikiwemo kutumia ishara ya mkono, sauti, na sura kufanya setting mbalimbali ikiwemo kupunguza sauti badala ya kutumia remote.
Smart
contents mfano Instagram, twitter, facebook na apps nyingine mbalimbali
ambapo unaweza kutumia Internet kuwasiliana kwenye mitandao mbalimbali
kama vile skype ambapo mnaweza kuonana zaidi ya watu watatu kwa wakati
mmoja.Ina music system yenye mziki mzito hapohapo hivyo ukiwa nayo huna haja ya kununua home theatre, pia faster speed squad core processor.
Digital tuner unaweza kupata local free channels zaidi ya 40 bila decorder na ukitaka channel za kulipia utatumia smart card ambayo unaiweka kwenye smart card slot nyuma ya TV yako.
Vilevile ukiwa na samsung smart phone unaweza kuiunganisha na TV ukaplay videos, music video games kutoka kwenye simu yako.
Unataka
kuwa karibu zaidi na stori zote zinazotokea na kuzipata kiganjani
mwako? stori kama hizi, siasa, muziki, michezo, movies na mengine?
jiunge kuwa mwanafamilia wa millardayo kwenye instagram.com/millardayo
twitter.com/millardayo na facebook.com/millardayo

CHANZO:MILLARDAYO
0 comments :
Post a Comment