
Mwanaharakati mmoja wa masuala ya wanawake nchini Ufaransa anasema kuwa, asilimia kumi ya wanawake nchini humo hupigwa kila mwaka huku mamia ya maelfu wakibakwa na kunyanyaswa kijinsia. Sambamba na kuwadia siku ya kimataifa ya kupambana na vitendo vya ukatili na utumiaji mabavu dhidi ya wanawake, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limetoa ripoti inayoonesha kuweko vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake. Ripoti hiyo inasema, asilimia 60 ya wanawake ulimwenguni hukumbana na vitendo vya ukatili na utumiaji mabavu au kubakwa. Hata hivyo la kusikitisha zaidi ni kwamba, hadi leo katika nchi 35 duniani kitendo cha kubakwa mwanamke hakihesahibiwi kuwa ni kosa na uhalifu. Zaidi ya wanawake milioni 603 wanaishi katika nchi ambazo utumiaji mabavu na ukatili dhidi ya wanawake ni mambo ambayo hayatambuliwi wala kuhesabiwa kuwa ni kosa na uhalifu. Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, kwa akali thuluthi moja ya wanawake duniani kila siku hupigha na wanaume ambapo utumiaji mabavu na ukatili dhidi ya wanawake umekuwa ukiteteresha nguzo ya jamii ya mwanadamu. Katika madola yanayodai kuwa vinara wa kutetea haki za binadamu ndiko vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake vinaposhuhudiwa kwa wingi. Takwimu zinaonesha kuwa, ukatili, unyanyaji na utumiaji mabavu dhidi ya wanawake unashuhudiwa zaidi katika nchi kama Uingereza, Marekani na Ufaransa. Kwa muktadha huo, kuna haja ya kuchukuliwa hatua za dhati na za kila upande kwa shabaha ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake.
CHANZO:KISWAHIIRIB
Blogger Comment
Facebook Comment