-->

PATA TASWIRA YA MCHEZO KATI YA MBEYA SANA NA RHINO RANGERS AMBAO UMEISHA KWA BAO 3-1

WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya maafande wa Rhino Rangers katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara ndani ya dimba lao la Sokoine jijini Mbeya.
Mbeya City sasa imetimiza pointi 39, moja zaidi ya Yanga SC inayoshuka kwa nafasi moja hadi ya tatu, baada ya kucheza mechi 21. Yanga imecheza mechi 17. Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa na Saad Kipanga mawili dakika za nane na 24 na lingine Deus Kaseke dakika ya 34, wakati Yohana Maurice alijifunga dakika ya pili kuipatia Rhino bao la kuongoza.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, afisa habari wa Mbeya City, Fredy Jackson  amesema kuwa mchezo ulikuwa mgumu sana kwani Rhino waliingia uwanjani kwa lengo la kutafuta pointi tatu.
“Rhino wameonesha upinzani mkubwa sana katika mchezo wa leo. Walidhamiria sana kupata ushindi, lakini ubora wa wachezaji wetu umetusaidia”. Alisema Fredy.







Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment