-->

MAAJABU YA MUNGU MVUA YANYESHA CALIFORNIA MASAA MACHACHE BAADA YA WAISLAM KUOMBA DUA MAALUMU YA KUOMBA MVUA

Saa chache baada ya Waislamu kusali na kuomba dua maalum kwa ajili ya mvua ili kupunguza ukame ambao tayari ulishaathiri maeneo ya California nchini Marekani hatimaye mvua imeanza kunyesha siku ya Jumapili februari 2,2014.

Swala hiyo ya kuomba mvua iliongozwa na Msomi na mwanzilishi wa Zaytuna College, Sheikh Hamza Yusuf na ilifanyika siku ya jumamosi baada ya swala adhuhuri katika viwanja vya Pleasanton Fairgrounds. 

Dua hiyo iliandaliwa na Baraza za la uhusiano la waislamu la San Francisco Bay Area inakadiriwa kuhudhuriwa na watu takribani 1,000.

Gavana Jerry Brown alitangaza hali ya dharula ya ukame mwezi Januari mwaka huu ambapo ni mwaka wa tatu wa hali ya ukame.

'Salatul Istisqa' ni swala maalum ya kuomba mvua iliyofundishwa na Mtume Muhammad pindi hali ya kutonyesha mvua inaposhamiri katika mji.

Waislamu nchini Marekani wakadiriwa kuwa kati ya milioni sita mpaka nane.


SOURCE:AHBAABUR
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment