
Aidha
mchezo huo umeshuhudiwa mashabiki wa Simba wakivunja viti vya Uwanja wa
Taifa kwa kumlaumu mwamuzi Juma Mgunda kuwa goli lililofungwa na Tambwe
halikuwa sahihi kwani Tambwe alishika mpira kwa mkono kabla ya kufunga
na pia tukio hilo lilipelekea nahodha wa Simba, Jonas Mkude kuonyeshwa
kadi nyekundu kwa kumpiga ngumi mwamuzi.
Pia
Simba imeendeleza rekodi ya msimu wa 2016/2017 kwa kutokufungwa mchezo
hata mmoja kati ya michezo saba iliyocheza mpaka sasa, ikishinda mitano
na kutoa sare mwili, kama utakuwa na kumbukumbu nzuri, msimu ulipita
Simba ilipoteza mchezo wa saba ilipokutana na Yanga na kufungwa goli
2-0.
Kwa
matokeo ya mchezo wa Yanga na Simba, Simba sasa imefikisha alama 17
ikiwa kileleni kwa msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Yanga
ikifikisha alama 11 ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa VPL.
SOURCE:DEWJI BLOG
0 comments :
Post a Comment