-->

KESI YA SHEKH PONDA YAPIGWA DANA DANA


KESI inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Ponda Issa Ponda, ambayo kwa sasa ipo kwenye hatua ya utetezi haikuendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro, baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutofika 
mahakamani hapo jana. 
Hakimu Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Mary Moyo anayesikiliza kesi
hiyo hakufika mahakamani kwa kile kihchodaiwa mahakamani hapo
kuwa amepatwa na dharura, hivyo kesi hiyo kuahirishwa hadi Aprili 2,
mwaka huu.
Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Morogoro, Maua Hamduni ndiye
aliyeahirisha kesi hiyo baada ya mtuhumiwa na mawakili wa pande zote
kufika mahakamani hapo na kuarifiwa kuwa hakimu anayesikiliza kesi
-
hiyo amepata dharura na hivyo kushindwa kuflka mahakamani.
Kwa mujibu wa Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Morogoro, Shehe Ponda
________
ataendelea kukaa rumande hadi siku hiyo atakapoletwa tena _____
mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya upande wa mashtaka kujibu hoja
_____
zilizotolewa na upande wa utetezi baacla ya kufungwa kwa ushahidi
ambazo ziliciai kuwa Shehe Ponda hakuwa na kesi ya kujibu.
Wakati kesi hiyo inaahirishwa askari polisi wenye silaha, mbwa pamoja
na mabomu ya machozi waliendelea kuimarisha ulinzi katika eneo
linalozunguka mahakama hiyo.
Hata hivyo, wafuasi wa Shehe Ponda walizuiwa kuingia ndani ya
mahakama na hivyo kubaki nje ya uzio wakiendelea kusoma Quran na
kufanya maombi licha ya mvua kunyesha.
Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka unaongozwa na mawakili wa
Serikali, Benard Kongola, Sunday Hyera na George Balasa, wakati
upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Juma Nasoro na Abubakar
Salimu.
Shehe Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri
halali ya mahakama, kutoa maneno yenye kuumiza imani za dini na
kushawishi watu kutenda kosa ambayo yote kwa pamoja anadaiwa
kuyatenda Agosti 10 mwaka 2013 katika uwanja wa shule ya msingi
kiwanja cha ndege, Manispaa ya Morogoro.
Mpckuzi blog
HABA1 MPYA 
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment