Baada ya watu kuwa na wasi wasi na uwepo wa mshambuliaji huyo katika
mchezo dhidi ya Chelsea kutokana kuoneka alitolewa huku akiwa na maumivu
makali katika mchezo wao waliotoka sare ya 2-2 jumatatu dhidi ya West
Bromich Albion, kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amethibitisha
kuwa mshambuliaji wake amefanya mazoezi na timu na yupo fiti kwa mchezo
huo.
Vile vile kocha huyo amesema kuwa kiungo wake Michael Carrick yupo
fiti tayari ila hatomuanzisha katika mchezo huo sababu ndo ametoka tu
katika majeruhi na inabidi aanze katika michezo midogo midogo ili azoee
kasi na siyo mchezo huo.
0 comments :
Post a Comment