
Sheikh Idriss aliuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake saa kumi na moja alfajiri ya kuamkia Jumanne wakati alipokuwa anaelekea katika Msikiti wa Swalihina ulioko takribani mita 50 tu kutoka nyumbani kwake.
Kwa muda mrefu Sheikh Idriss alikuwa mwenyekiti na Imamu wa Msikiti wa Sakina mjini Mombasa kabla ya kuondolewa kwa lazima na vijana wenye itikadi kali.
Kamishna wa Mombasa Nelson Marwa amesema kuwa, polisi wameekwa katika maeneo mbali mbali ili kuhakikisha usalama kwa raia unalindwa.
Mwandishi wa Radio Tehran mjini Mombasa, Seifullah Murtadha ametuandalia ripoti ifuatayo:
0 comments :
Post a Comment