
Jihad al Laham, Spika wa Bunge la Syria ametangaza kuwa, Assad ameshinda kwa asilimia 88.7 ya kura kwa kupata kura 10,319,723 kati ya kura 11,634,412 zilizopigwa.
Kwa upande wake, Mahakama Kuu ya Katiba ya Syria imetangaza kuwa, asilimia 73.42 ya wananchi milioni 15.8 wa Syria waliotimiza masharti ya kupiga kura walishiriki kwenye zoezi hilo.
Mahakama hiyo imeongeza kuwa, hakuna malalamika yoyote yaliyowasilishwa kutoka kwa wagombea wengine wawili wa kinyang'anyiro hicho.
Baada ya kutangazwa matokeo hayo, wananchi wa Syria wamemiminika mabarabarani kwa nderemo na vifijo kusherehekea ushindi huo.
Wakati huo huo timu za kimataifa zilizoshuhudia uchaguzi huo wa rais wa Syria zimesema kuwa ulikuwa huru na wa wazi. Bw. Bashar al Assad ataendelea kuwa rais wa Syria kwa kipindi kingine cha miaka 7.
0 comments :
Post a Comment