



BAADA
kukaa Miaka 9 bila Kombe lolote, baada kutwaa FA CUP Mwaka 2005, Leo
hii Uwanjani Wembley, Jijini London, Arsenal wamefanikiwa kubeba FA CUP
walipotoka nyuma kwa Bao 2-0 ndani ya Dakika 8 za kwanza na kushinda 3-2
katika Dakika 120 za Gemu.
Hadi Dakika 90, Bao zilikuwa 2-2 na
Dakika za Nyongeza 30 zikaongezwa na Aaron Ramsey kuifungia Arsenal Bao
la ushindi katika Dakika ya 109.
Hull City walitangulia kwa kuongoza Bao 2-1 katika Dakika 8 za kwanza tu na Arsenal kupata Bao la Kwanza Dakika ya 17.
Arsenal walisawazisha kwenye Dakika ya 71 na Gemu kumalizika 2-2 katika 90 za Mchezo na ndipo zikaja Dakika za Nyongeza 30.
0 comments :
Post a Comment