
Alipofika kwa mgonjwa huyo mhubiri huyo alianza kwa kunena kwa lugha isiyofahamika kisha kurejea katika lugha ya kiswahili kwa kumuombea mgonjwa huyo aweze kupona maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.Kabla hajamaliza kumuombea mgonjwa huyo,mgonjwa alijitahidi kunyanyuka kisha kuandika jambo kwenye karatasi na kumpa mhubiri huyo.Yule mhubir aliichukua karatasi ile bila ya kuisoma na kuiweka kwenye mfuko shati na kuendelea na maombi yake kama kawaida.Kipindi anamaliza maombi akashangaa kuona mgonjwa akaanza kukoroma kisha jasho kutoka kwenye paji la uso na miguu kuwa ya baridi....ikabidi amuite daktari,daktari alipokuja alikuta mgonjwa ameshafariki.
Mhubiri yule alifanikiwa kuhudhuria mazishi ya mgonjwa yule yaliyofanyika siku moja baada ya kifo cha mgonjwa yule.Baada ya mazishi mhubiri aliingiza mkono kwenye mfuko wa shati wa mbele na kukuta karatasi iliyosomeka kwamba
MHUBIRI SAMAHANI HAPO ULIPOSIMIMAA UMEKANYAGA MRIJA WA HEWA HIVYO NASHINDWA KUPUMUA....
Ilimuuma sana baad ya kugundua kwamba yeye ni sehemu ya kifo cha mgonjwa yule lakini hyo haikusaidia kumrejesha maiti kwenye uhai wake
FUNZO:tuwe na desturi ya kusoma karatasi mbali mbali tuanazopewa na sio kuzipuuza
Usitizame hadhi ya mtu anaekupa taarifa fulani kwenye karatasi
HEBU TIRIRIKA NA WEWE UMEJIFUNZA NINI KWENYE KISA HIKI
0 comments :
Post a Comment