
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amerejesha matumaini ya Manchester United kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuanza mazoezi kwa ajili Robo Fainali ya pili dhidi ya mabingwa watetezi, Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena kesho.
Rooney
alikosa mechi ya Ligi Kuu England United ikiifunga mabao 4-0 Newcastle
mwishoni mwa wiki kutokana na maumivu ya mguu, lakini sasa kuna
uwezekano kesho akacheza
Ryan
Giggs pia alifanya mazoezi baada ya kukosa mechi dhidi ya Newcastle,
lakini Marouane Fellaini, ambaye alitolewa nje Uwanja wa St James Park
baada ya kuumia na Rafael hawakushiriki mazoezi leo.
Baada ya sare ya 1-1 nyumbani, United sasa wanatakiwa kushinda ugenini dhidi ya Bayern ili kutinga Nusu Fainali.

Rooney alishiriki mazoezi kikamilifu

Rooney ameonekana kusahau kabisa kuhusu maumivu

Rooney ameonekana yuko fiti kwa ajili ya mchezo huo

Kocha wa Manchester United, David Moyes ameonekana kufurahia kurejea kwa Rooney
0 comments :
Post a Comment