
Mamake mwathiriwa alimzaba kofi mtuhumiwa na kisha kumasamehe dakika chache kabla ya kunyongwa
Mtu mmoja aliyehukumiwa kifo kwa
kunyongwa nchini Iran baada ya kupatikana na hatia ya mauaji, ameponea
chupuchupu baada ya kusamehewa na mamake mwathiriwa.
Mama huyo alimsamehe mtuhumiwa dakika chache tu kabla ya kuwekwa kamba shingoni.Picha za tukio hilo zilipigwa moja kwa moja na mpiga picha mmoja aliyenasa kila hatua ya tukio hilo ambalo liliwashangaza wengi nchini Iran na duniani kote.

Balal alimuua kwa kumdunga kisu Abdollah Hosseinzadeh miaka saba iliyopita
Bilal alifikishwa katika sehemu ya kunyongewa akiwa amefunikwa macho yake tayari kwa hukumu kutekelezwa siku ya Jumanne.
Lakini dakika ya mwisho kabla ya kunyongwa, mamake mwathiriwa Samereh Alinejad, alimwambia kuwa amemsamehe baada ya kuhutubia umati uliofika kushuhudia hukumu hiyo , kisha akamzaba kofi Bilal kabla ya Bilal kunusurika kifo.

Samereh Alinejad, mamake marehemu Abdollah Hosseinzadeh, alimzaba kofi Balal dakika za mwisho alipokuwa anasubiri hukumu

Kisha alimuondoa kamba shingoni akisaidiwa na mumewe.

Kabla ya mama huyu kumsamehe Balal alihisi hisia kali baada ya kukumbuka kifo cha mwanawe
0 comments :
Post a Comment