-->

HAWA NDIO MANCHESTER UNITED KAMA ULIKUWA HUWAJUI HEBU WASOME HAPA

Kati ya mwaka 1922 hadi mwaka 1940 kilikuwa ni kipindi kigumu kwa Manchester United. Ilikuwa ni kawaida kwake kushuka daraja kila ilipojitutumua kupanda ligi huku mwaka 1931 ikifilisika kabisa.

Kati kati ya miaka ya 1940 ndipo ilipoanza kukijenga kikosi chake cha ushindi na matunda yalianza kuonekana miaka ya 1947, 48 na 49 ambapo katika miaka hii ilimaliza ligi kwenye nafasi ya pili huku mwaka 1948 ikishinda kombe la FA na kuwa timu ya kwanza kutoka Uingereza kucheza michuano ya Ulaya.

Timu iliendelea kuimarika zaidi chini ya kocha Matt Busby ambapo katika miaka ya 1952, 1955 na 1956 ilimaliza ligi katika nafasi ya kwanza.
Hii ndio Manchester United!

Mwaka 1958 ilikuwa ikishiriki mashindano ya Ulaya, ilipokuwa na kikosi chake chenye wastani wa umri wa miaka 24 kwa mchezaji. Kikosi ambacho kilikuwa maarufu kwa jina la Busby Babes.

Wakiwa wametoka kifua mbele kwa ushindi wa 2:1 nyumbani Old Trafford dhidi ya Red Star Belgrade ya Yugoslavia ambayo ni Serbia ya sasa. Mechi ya marudiano iliyochezwa mjini Belgrade matokeo ilkuwa ni sare ya goli 3.

Tarehe 6.2.1958 wakiwa wanarejea nyumbani na ndege maalumu iliyokuwa na jina la Lord Burghley ikiwa imebeba wachezaji wa United, mashabiki, baadhi ya viongozi na waandishi wa habari. Ndipo ilipotua mjini Munich katika iliyokuwa Ujerumani magharibi kuongeza mafuta.

Ndege ilipojaribu kupaa mara kadhaa ikaferi , ikagonga baadhi ya majengo na kulipuka. Wachezaji 8 wa kikosi cha kwanza wa Manchester United walikufa kutokana na ajali hiyo huku wengine kadhaa wakipata majeraha yaliyowafanya wasiweze kuendelea na soka tena.

Wachezaji waliopata umauti kutokana na ajali hiyo ni ~

1. Geoff Bent
2. Roger Byrne
3. Eddie Colman
4. Mark Jones
5. David Pegg
6. Tommy Taylor
7. Liam "Billy" whelan
8. Duncan Edward ambae alijeruhiwa vibaya na kufia Hospitali baada siku 15 yaani February 21.

Sir Matt Busby alibidi abaki hosptali kwa miezi mitatu zaidi kwa ajili ya tiba. Hata alipopona alihamia nchini Uswisi alikaa kwa mwaka mmoja huku akizimia kuachana na masula ya soka.

Wakati huo timu ilibaki chini ya kocha msaidizi, ikiwatumia wachezaji vijana mwaka huo iliweza kufika fainali ya kombe la FA.
Hii ndiyo Manchester United!

Baada ya kushauriwa sana Sir Matt Busby aliamua kurudi kuisuka upya timu kwa kutumia wachezaji vijana.

Kwa hakika lilikuwa ni anguko kubwa kwa timu na hali kuhuzunisha.

Ilibidi kusubiri kwa miaka 7 kikosi kipya cha Matt Busby kurudi kwenye hali yake ambapo Mwaka 1965 na 1967 timu ilichukua ubingwa wa Uingereza na mwaka 1968 miaka 10 baada ya ajali, ikiwatumia vijana kama George Best na Denis Law huku wachezaji waliokuwepo wakati wa ile ajali wakiwa ni Bobby Chalton na Bill Foulkes pekee. Waliweza kushinda ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza!
Hii ndiyo Manchester United!

Leo ni siku ya kuwakumbuka mashujaa wetu waliofari kwa ajali ya ndege jijini Munich.

Siku zote Manchester United wanaamini kwamba tukiwa uwanjani tukicheza na kushinda basi wale mashujaa wanafurahi kutoka huko waliko.
IMEANDIKWA NA:DAVID PETER
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment