-->

HABARI YA KUSIKITISHA,MWANAMKE AMUUA MUMEWE KWA KUMPIGA NA JEMBE KICHWANI

 
Watu watatu wafariki dunia mkoani Iringa katika matukio manne tofauti likiwemo la Ponsian Vakuka (37) mkulima wa Ihowanza kufariki dunia baada ya kukatwa na jembe kichwani.
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 27 january majira ya saa 1:30 jioni.
 
Mungi alisema kuwa marehemu alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili na mke wake aitwaye Mwamvita Tinda (35) ambapo chanzo kilisemekana mwanamke huyo alikuwa amelewa wakati akifanya mauaji hayo, hata hivyo mtuhumiwa amekamatwa.
 
Wakati huohuo watu wawili wakazi wa Lulanda kata ya Ihanu tarafa ya Ifwagi wilaya ya Mufindi waliuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za kishirikina.
 
Mungi alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 2 februari majira ya saa 6 kamili mchana ambapo aliwataja watu hao ni Alutal Kihongole (95) pamoja na  Boscow Masonda (85) wote ni wakulima, hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.
 
Wakati huohuo Elias Ngope (78) mkazi wa Kisonga tarafa ya Pawaga alikutwa akiwa amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye bwawa la maji akiwa anaoga, chanzo cha tukio hilo ni marehemu alikuwa anaugua ugonjwa wa kifafa.
 
Mbali na matukio hayo ya kusikitisha, Kamanda Mungi alisema watu wasiofahamika waliiba pikipiki yenye namba za usajili T. 507 CBE aina ya Sky mark ya rangi nyeusi yenye thamani ya shilingi 1,800,000/= mali ya Simaitoni Kionza (33) mkazi wa Ipogoro, ambapo watuhumiwa wanatafutwa.
 
SOURCE:DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment