
Taarifa kutoka Ikulu ya Rais Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja amekamatwa. Mshukiwa huyo amejeruhiwa na anapokea matibabu hospitalini.
Wanamgambo wa Al Shabaab wanasema kuwa Kenya haikuchukulia kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka wanajeshi wake nchini humo kupambana dhidi yao.
Kundi hilo limesema limekuwa likitoa onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa vikosi vyake nchini Somalia, athari zitakuwa mbaya mno.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab limesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waisilamu wasio na hatia nchini Somalia.
Taarifa hiyo ya Twitter ilisema kuwa Shambulio la Westgate ni tone katika bahari tu ya mfano wa yanayowakumba wasomali waisilamu nchini Somalia.
HABARI HII IMENUKULIWA KUTOKA BBC SWAHILI
0 comments :
Post a Comment