-->

TAJIRI NAMBA MOJA AFRIKA ALIKO DANGOTE KUINUNUA ARSENAL

Aliko Dangote, mtu tajiri zaidi barani Afrika,ana mpango wa kuinunua klabu ya Arsenal kutoka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne.

Dangote ambaye ni raia wa Nigeria ana thamani ya dola bilioni 10.9,kulingana na orodha ya watu tajiri duniani iliotolewa na runinga ya Bloomberg mjini New York siku ya Jumatano, alitangaza nia yake ya kukinunua klabu hicho mwaka uliopita.

Alisema kuwa anasubiri biashara zake kuimarika pamoja na uwekezaji wake wa ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha kusafisha mafuta kabla ya kukinunua klabu hicho.

''Hakuna tatizo kwamba nitainunua klabu hiyo, na si tatizo la fedha," alisema Dangote katika mahojiano na runinga ya Bloomberg .

''Pengine miaka mitatu au mine. Suala ni kwamba tuna changamoto nyingi. Ninahitajika kukabiliana nazo mwanzo baadaye nitaangazia suala la ununuzi huo''.

Dangote ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal amepoteza kiasi cha dola bilioni 4.4 mwaka huu kutokana na kushuka kwa thamani ya sarufi ya Nigeria.

Utajiri wake mwingi upo katika kiwanda cha saruji kilichopo mjini Lagos.

Iwapo atainunua timu hiyo basi atakuwa mtu wa kwanza kutoka barani Afrika kumiliki timu iliyopo katika Ligi Kuu ya England
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment