-->

BIASHARA YA NGONO JINSI INAVYOIHARIBU MANISPAA YA MOROGORO(SEHEMU YA PILI)

Katika sehemu ya kwanza ya makala hayo tuliishi kwa kuona Naibu Meya mstaafu Lidya Mbiaji akieleza namna ya tabia  hatarishi zinachangiwa na wamikili wa kumbi za sterehe juu ya biashara ya ngono namna ilivyovatikisa Morogoro sasa tuendelee na habari hiyo......

Na Juma Mtanda, Morogoro.

Mbiaji alisema kuwa tabia hatarishi zinachangiwa na wamikili wa kumbi za sterehe ambapo machangudoa wamekuwa wakifanya biashara zao za kuuza miili na hali hiyo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nao wamejiingiza huku kundi lingine la wafanyakazi wa ndani na wanawake waliopo ndani ya ndoa wakiwa katika kundi.

Wanawake walioolewa na wafanyakazi wa ndani hawana vituo maalum vya kuuza ngono isipokuwa kundi lingine la wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, wenyewe wanaungana na kundi lililoshindikana katika biashara hiyo katika maeneo maalum katika kumbi za sterehe.
JAMII NA VIONGOZI WANAFUMBIA MACHO.
 “Baada ya utafiti wetu maeneo mbalimbali, tuliwaita wafanyabiashara na kuwaeleza hali halisi ya maambukizi mapya namna mkoa wa Morogoro inavyoongezeka kasi kwa wagonjwa wapya lakini hali ni ile ile na wenye thamana ya kuwafutia leseni wafabiashara kumbi za sterehe wamekaa kimpya baada ya kuwasilisha ripoti yetu lakini ni kweli kumbi hizo zinazochangia kufuga machagundoa.”alisema Mbiaji.
Alisema kuwa achilia mbali kumbi za sterehe kuficha kundi hilo kwa nyakati zote za mchana na usiku lakini hao wenyewe makahaba, machangudoa, wasenge na wengine wamekuwa wakiitaka serikali iwatambue ili kuepukana na unyanyasaji kutoka kwa madaktari pindi wanapoumia kutokana na maumbile makumbwa sehemu za siri ama haja kubwa.
“Kwanza wenyewe hao machangudoa na mashoga wanataka serikali itunge sheria za kuwatambua ili hata hospitalini pindi wanapoenda kutibiwa wasinyanyapaliwe na madaktari pindi wanapoumizwa wakati wa ngono au kuingiliwa kimaumbile kwani wamekuwa wakiumia sehemu za haja kubwa na maumbile makubwa na wamekuwa wakiyasema hayo wakati tunapowaita kuwapa semina za maambukizi ya ukimwi kwa makundi hayo.”alisema Naibu Meya huyo mstaafu.
Licha ya kutaka serikali itungwe sheria za kuwatambua na shughuli zao hizo lakini wanaitaka serikali inunue vilainishi (mafuta maalumu na kondom maalum kwa kazi hiyo) ili mashoga na machangudoa wawe wanaitumia ili kuepusha kuumia wakati wa kutoa huduma kwa wateja wao.
WIKIENDI HUCHUKIWA NA MAKUNDI HAYO.
Mbiaji aliendelea kufichua siri za mashoga na machangudoa wauza ngono kuwa siku hizo za jumamosi na jumapili pamoja na siku za sikukuu zimekuwa shida kwao kutokana na kukosa wateja wa uhakika kutokana na wateja wao ambao ni wanaume wa watu kutokwenda kazini  kukosa mapato ya kutosha.
Manispaa kuchukua hatua ya kubidhiti.
Baada ya kuyatambua makundi hayo ili kuachana na kazi hiyo, halmashauri ipo tayari kutoa mikopo ya liba nafuu ili  kuwakopesha pesa ili wafanye biashara halali huku ikiwapigia magoti wamiliki wa kumbi za sterehe kusaidia kuwashaswishi makundi hayo kuachana na kazi hiyo na kujiingiza katika biashara za ujasiliamali.
“Wazazi nao wanapaswa kuwa makini na malezi ya watoto wa jinsia zote hasa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kuwadhibiti ili wasizurule ovyo nyakati za jioni na usiku kwani mwanya huo hutumiwa vizuri na watoto wenye kuiga tabia za kimaghalibi kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kutimiza majukumu ya malezi.”alisema.
Mbiaji alisema kuwa kinachoumiza zaidi ni kusikia wanafunzi wa shule za msingi wakijiingiza katika biashara hiyo kwani ni kundi ambalo lilikuwa halijaingia katika vitendo vya uuzaji wa ngono lakini sasa hivi tayari nao wameingia rasmi kutokana na dada zao wa sekondari kujiingiza.
Tulitoa pendekezo.
Mbiaji alisema kuwa baada ya kuunda kamati iliyoundwa kufuatia makundi yaliyovamia Morogoro ilitoa mapendekezo ya kufutiwa leseni za biashara katika zile kumbi za sterehe zilizokiuka taratibu na sheria za nchi lakini wenye mamlaka na suala hilo wamekaa kimya na tatizo kuendelea kukua siku hadi siku.
“Kazi ya kuyatambua makundi hayo ilifanyika kwa upelelezi wa hali ya juu kwani ilishirikisha viongozi wanne wa dini ya kiislamu na kikristo, madiwani watatu, watendaji watatu wa halmashauri nikiongoza jahazi mimi mwenyewe na watu waliotuona walishindwa kutofautisha kwani wanawake wote tuvaa nguo fupi na watu walivaa kihuni ili kulingana na uhalisia na mienendo ya machangudoa huku wanaume katika msafara huo wakifanana na tabia za mashoga.”.alisema Mbiaji.
Ni mambo ya aibu yaliyoonekana katika vyumba vya makahaba baada ya kushuhudia makundi hayo kwa kuwaona wanaume wanne na wanawake wanne wakiwa chumba kimoja, vitanda viwili wakifanya vyao achilia mbali waliokuwa wakifanya kazi hiyo kitandani wengine walikuwa wameshika ukuta lakini ni lazima ulipia fedha mlangoni kiasi cha sh 1,000.
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA MWANZOMGUMU KATA YA MWEMBESONGO.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Mwanzomgumu kata ya Mwembesongo Mmanispaa ya Morogoro, Saidi Omari Kamba (66) yeye alisema kuwa biashara ya makahaba ipo katika eneo lake la mtaa wa Mwanzomgumu sehemu ya Msamvu Itigi na sasa biashara hiyo inatimiza mwaka wa pili.
Kamba alisema kuwa tetesi za wanawake hao kufanya biashara ya ngono zimemfikia katika ofisi yake kutoka kwa wazazi wakilalamikia tabia zinazofanywa na machangudoa hao kuwa wamekuwa kero hasa kwa maadili yanatokana na uwepo wao jirani na makazi ya watu ambayo kumetapakaa watoto wadogo ambao ni rahisi kuiga tabia hiyo.
“Mimi kama mwenyekiti baada ya kupata taarifa za uwepo wa makahaba nilifanya uchunguzi na kubaini ukweli na kingine nilichoelezwa kuwa kuna tetesi za wanawake hao kupangisha moja ya nyumba na kulala kisha giza likianza kuingia, kujisogeza eneo la Msamvu Itigi na kuanza kuuza miili yao kwa  wanaume kwa lengo la kupata ujira wa fedhaa.”alisema Kamba.
Kamba alisema kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na kundi kama hilo lakini kundi hilo lilikuwa limejisitiri katika nyumba maalumu na athari zake zilikuwa ndogo sana tofauti na sasa hivi ambako wanawake hao wamekuwa wakiuza miili yao sehemu ya wazi tena hata watoto hawajalala.
“Tumefanya vikao vingi na wazazi juu ya namna ya kuwaondoa wanawake hao lakini serikali ya mtaa haina ubavu wa kuwaondoa lakini suala hili tumefikishaa katika ngazi za juu lakini na wao wamekaa kimya sasa kero imebakia kupokea malalamiko kila kukicha kutoka kwa wazazi.”alisema Kamba.
MFANYABIASHARA WA KWANZA MSAMVU.
Leonard Mwofuga yeye ni mfanyabiashara mwanzilishi ambaye alikuwa mfanyabiashara wa kwanza kuweka kibanda cha biashara mwaka 2000 hadi leo mwaka 2014 anaeleza historia ya eneo la Msamvu stendi na namna machangudoa walivyovamia.
Mwofuga anasema kuwa februari mwaka 2000 ndiye yeye alianza kuweka kibanda cha biashara baada ya serikali kuhamisha stendi kuu ya mabasi yaendapo mikoani katikati ya mji na kuhamishia Msamvu ambao sasa panajulikana kama Msamvu Itigi na jina la Itigi lilitokana na mama lishe wenyeji wa Itigi kutoka Singida waliomiminika mmoja baada ya mwingine hadi leo eneo hilo limesheheni wafanyabiashara wa kila aina.
Eneo la Msamvu stendi kabla ya stendi kuhamishiwa eneo hilo lilivuma kwa majina ya Msamvu kwa Mela, Msamvu kwa Lupilo, Msamvu Hay Way, Msamvu BP lakini majina hayo yalipungua nguvu tangu mwaka 2012 baada ya mfanyabiashara mmoja wa vinywaji kuhamia eneo hilo na kundi la machangudoa, makahaba, wasenge na mashoga akihama nao kutoka katikati ya mji na kuhamia eneo hilo ambalo kwa sasa linajulikana kama Msamvu Itigi.
Neno Itigi lilivuma kutokana na mama lishe waanzilishi wa kuuza chakula akiwemo mmoja wao aliyefahamika kwa jina la mama Mbarouku akitokea katika mji mdogo wa Itigi Singida sambamba na wahudumu wake waliokuwa na jukumu la kuhudumia wateja wake wa chakula wakitokea katika mji mji huo mdogo wa Itigi kwa mwaka 2001.
“Nakumbuka vizuri maana halisi ya jina la Itigi linatokana na akinamama wauza chakula kutoka mji mdogo wa Itigi mkoani Singida lakini sasa hivi limebadilika maana yake, kwa sababu sasa hivi Itigi ya Msamvu Morogoro, tafsiri yake ya haraka ni Itigi inayopatikana machangudoa na siyo Itigi ile ya mwaka 2000 ilikuwa na maana ya kupata huduma ya kulala bora na safi kwa wageni mbalimbali wakiwemo wasafiri na madereva.”alisema Mwofuga.
Zamani neno Itigi ilivuma kwa nia njema tu tena ikiwa na maana mama lishe na wafanyakazi wao wakitoka Itigi mkoani Singida lakini sio kwa sasa hivi neno Itigi linavuma kutokana na kushamili kwa kila aina ya wauza ngono wa kila rika kuvamiwa hali iliyosababisha usumbufu wa kila aina sio kwa wafanyabiashara tu bali hata jamii inayoishi jirani na eneo hilo.aliongeza Mwofuga.
“Kwa mfano mimi, familia yangu kuanzia watoto wa kike, wavulana na mama yao hata majirani zangu nimewapiga marufuku kutotembelea eneo la biashara yangu ama eneo la Msamvu Itigi na hii inatokana na hali halisi kwani kimsingi sio mzuri kimaadili kutembelewa na mtu anayekuheshimu, acha mambo haya yaishie kwangu mimi kwa sababu nina saka pesa kama unavyojua pesa husakwa katika mazingira magumu ikiwemo haya.”alisema Mwofuga.
Eneo hili lina karaha ya kila aina hasa jua likizama kwani utashuhudia utitiri wa machangudoa, wasenge, makahaba na mashoga wakianza kutanda na kujibaza kando ya malori na nguo zao za nusu utupu wakiwasubiri wanaume kuwachukua na kwenda kufanya nao ngono.alisema mfanyabiashara huyo.
Mfanyabiashara huyo alisema kuwa karaha inayopatikana eneo hilo ni pamoja na kuzagaa ovyo mipira ya kiume, kukosa wateja wa kununua bidhaa za wafanyabiashara maeneo hayo hasa wale viongozi wa serikali na wateja wengi wanaojiheshimu na kero za hapa na pale kwa baadhi ya wateja wao kuibiwa mali baada ya kuwekewa madawa ya kulevya katika vinywaji na machangudoa hao.
“Mwandishi kama utapata muda wewe njoo eneo hili la Itigi hapa Msamvu saa 4 usiku  utaona mwenyewe kinachofanyika na utakili niliyokueleza yote yana ukweli mtupu na hapo nyuma kuna vibanda vinavyotumiwa na machangudoa wa bei ya chini na wale wenye machangudoa wenye kiwango cha juu humpeleka mteja wao katika vyumba vya kulala wageni katika eneo hilo hilo.”alisema Mwofuga.
Alisema kuwa machangudoa hao wameambukiza tabia mbaya kwa wafanyakazi wa majumbani kuacha kazi na kuingia katika biashara hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya kuingia kwa mwajili wake wakitokea vijijini kwao.
Mwofuga alitoa wito kwa serikali kuiangalia eneo hilo la Msamvu Itigi kwa jicho la pili kwa kufanya operesheni ya nguvu ya kuwaondoa machangudoa hao eneo hilo lililozungukwa na jamii ili vijana wa kike na wavulana wasiendelee kuwa na vishawishi vya kuingiza katika vitendo vya kujiuza na ushoga vingine viwango vya ongezeko la ugonjwa wa ukimwi utaendelea kuwa juu mwaka hadi mwaka na pengine kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwa maambukizi ya Ukimwi.
Mwofuga alisema kuwa kakundi hayo sio wote wanaingiliwa kwa kutumia mipira ya kiume na wanaume bali wapo wanaoingiliwa bila mipira ya kiume kutokana na sababu moja ama nyingine.
Alitaja sababu hizo za kuingiliwa machangudoa na wanaume kinatokana na ukweli kwamba wakati mungine baadhi yao hao machangudoa hukaa muda mrefu bila kupata mteja na mteja wake wa kwanza kumlazimisha kufanya naye ngono bila kinga hapo ndipo penye shida na kulazimika kukubali ili kuondoa mikosi siku husika.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu tangu kufuatilia mienendo ya machangudoa hao imegundua wanaume wanaofika eneo hilo la Msamvu Itigi kutozwa fedha kwa viwango tofauti kutokana na aina ya changudoa waliogawanyika katika makundi mawili.
Makundi hao ni yale yanayotoa huduma ya ngono ya kuanzia sh2,000 hadi sh 4,000 mteja akilazimika kuingizwa katika kibanda ili akidhi haja zake katika godoro lililotandikwa chini ya ardhi huku mmiliki wa kipanda hicho akimtoza changudoa kiasi cha sh1,000 kila mteja atayeingia naye vibanda vilivyopo nyuma ya vibanda vya biashara wa chakula, vinywaji na n:k.
Kundi lingine ni lile la machangudoa wa hadhi ya juu ambao wao hutoza dau la sh5,000 na kuendelea na kumpeleka mteja wao katika vyumba vya kulala wageni, nyumba ambayo ipo eneo hilo lakini ni hatari endapo watagundua mteja wao ana pesa na vitu vya thamani kwani wanaweza kumdhuru kwa kumwekea madawa ya kulevya katika vinywaji ama kumlaghai kwa kumnyonya matiti yake kabla ya kufanya ngono.
MJUMBE WA BARAZA LA MASHEKHE MKOA WA MOROGORO.
Mjumbe wa baraza la mashekhe mkoa wa Morogoro, Shekhe Ally Omari Ngarawa alieleza kuwa yeye kama kiongozi wa dini ya kiislaamu alisikia taarifa hizo baada ya siku moja kudhuria mchezo wa dhumna uliokuwa ikichezwa eneo la soko la mkoa wa Morogoro majira ya jioni.
Ngarawa alisema kuwa ni suala la aibu kwa wao kama viongozi kufumbia macho na kuwaacha makahama wakiendelea kufanya biashara ya ngono zaidi ya miaka miwili sasa eneo la Itigi na maeneo mengine.
“Siku moja nilisikia wanamichezo wa mchezo wa dhumna wakiongea juu ya biashara ya ngono Itigi lakini nilistuka na kutega sikio kusikia maneno hayo na sikuweza kuchangia mada hiyo na nilichofanya nilifanya utafiti wangu kwa wiki mbili ili kubaini ukweli kwa kuchunguza kile nilichosikia na kweli nilibaini ukweli huo.”alisema Ngarawa.
Ni kweli ngono inafanyika tena bila kificho, mwanaume akifika hilo eneo la Itigi huchagua mwanamke anayempendeza naye na kupatana bei kati ya sh3,000 hadi sh5,000 na wakati mwingine hufikia kiasi cha sh10,000 kutokana na matakwa ya mteja husika.aliema Ngarawa.
Ngarawa alifafanua kuwa katika utafiti wake huo aligundua kuwa bei hizo hutozwa kwa huduma mbalimbali kuwa kuanzia sh3,000 hadi sh5,000 mteja hutozwa kwa kufanya ngono upande wa mbele na kufanya ngono kinyume na maumbile mteja hutozwa sh10,000 lakini ni lazima mwanaume avae mpira wa kiume.
Alifafanua kuwa katika biashara hiyo wale wanaotumia kinga kwa maana ya kuvaa mipira ya kiume hupunguziwa bei na wale wanaume ambao hawataki kuvaa mipira ya kiume hujikuta wakitozwa fedha nyingine sambamba na wale wanaowaingilia wanawake hao kinyume na maumbile kujikuta wakitozwa pesa nono.
Alieleza kuwa lengo la kufanya utafiti huo alikuwa na maana ya kufikisha ujumbe kwa waumini wa dini ya kiislamu nyakati za ibada za ijumaa ambako waumini hufika msikitini kwa uwingi na kutoa mahubiri mara nne ndani ya mwezi moja.
Kwa mujibu wa shekhe huyu ambaye ni mwakilishi wa shekhe wa mkoa wa Morogoro alianza kufanya utafiti februari mwaka huu lengo likiwa kutoa mafundisho ya namna ya kutojiingiza katika ngono kwani hata kitabu kitakatifu cha msahafu kinakataza kutokaribia uzinifu kwani inamfanya binadamu kupata dhambi na kumwingiza katika hukumu ya moto mbele ya mwenyezi mungu.
Ngarawa alisema kuwa baada ya utafiti huo amegundua kuwa hali hiyo ya makahaba inatokana na malezi mabaya kutoka kwa wazazi wao hasa maisha magumu hivyo serikali inawajibika kuwaondoa machangudoa sehemu zote za mkoa wa Morogoro.
Baada ya kufanya kazi hiyo serikali hiyo inapaswa kuwakusanya katika vikundi na kuwapatia mitaji ili waweze kufanya biashara na hapo watakuwa wamerahisisha kupunguza adha ya kupata magonjwa ya maambukizi kama ukimwi.
Hata wakati wa operesheni ya kuwaondoa katika madanguro lazima washirikishe makundi mbalimbali ya watetezi wa haki za wanawake kama Tamwa, TGNP, Fame Act, haki za binadamu na haki za watoto na wengine ili kuondoa msuguano ndani ya jamii.

RAIS KIKWETE AELEZA KUPATA UKIMWI NI JAMBO LA KUJITAKIA.
Rais Jakaya Kikwete akihutubia wananchi wa mkoa wa Morogoro katika uwanja wa jamhuri alieleza umma wa watanzania kuwa ugonjwa wa ukimwi unatafutwa na sio ugonjwa wa bahati mbaya.
“Badilisheni tabia ukimwi ni ugonjwa wa kujitakia kwa baadhi ya watu, sio sifa nzuri kabisa, unausaka ukimwi kwa kupanga muda, saa, dakika na sehemu ya kukutana ili kufanya ngono sasa hapo utasema mtu ameupata kwa bahati mbaya ?.alisema Kikwete.
Kikwete pia alitumia mwanya huo kuwakalipia viongozi kwa kuwata kuacha woga na ulegevu katika kusimamia sheria za kulinda zinazoongoza nchi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro (RPC) Leonard Paulo akizungumza na mwandishi wa makala hayo ofisini kwake, aliyetaka kupata nini jeshi hilo linafanya juhudi za kunusuru jamii mzima inayozungukwa na kumbi za sterehe ambazo zimekithiri kwa vitendo vya kupomoka kwa maadili ya mtanzania vinavyofanywa na vitendo vya wasichana, wanawake na mashoga kuuza ngono mjini hapa.
Paulo alieleza kuwa yeye kwanza ndiyo anapokea taarifa kutoka kwa mwandishi huyu hivyo kitu cha msingi kwake ni kulifanyia kazi kisha kumpatia majibu sahihi baada ya yeye kuchunguza na siku ya siku ilete tija kwa jamii ya Morogoro na taifa kwa ujumla.
"Nimekusikiliza na nimekuelewa nini unataka kufahamu juhudi za jeshi la polisi katika kuinusuru jamii na maporoko ya maadili kwa jamii ambazo zinazungukwa na kumbi za starehe, nalifanyia kazi ili nami nijiridhishe kutokana na kauli yako ili nikupe taarifa iliyosahihi kwa lengo la kuelemisha jamii."alisema Kamanda Poulo.
Huu ndiyo mwisho wa makala hayo baada ya kufichua uovu unaofanywa na wanawake na wanaume kufanya biashara ya ngono.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment