
Marehem Jaffar Siraji alifariki dunia jana usiku katika hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na maumivu makali ya kichwa
Jaffar Siraj alisoma hotba na kujumuika na waislam kwenye EID DHUHA katika viwanja vya K/NDEGE. Jaffar Siraji atakumbukwa kwa wasikilizaji na watazamaji wa Radio Imaan na Tv Imaaan kwenye kipindi cha MWANGAZA WA JAMII


Al akhy Jaffar Sirak katika zama za uhai wake
Historia inaonyesha Jaffar Siraj alisoma elimu ya stashahada katika chuo cha kiislam cha Ubungo Islamic Teacher's College ambako alihitimu mwaka 2004 na kisha akasomesha Msamala Muslim Songea na baadae Matangini Islamic Dar, akajiunga na Chuo cha Waislamu Morogoro wakiwa ndio Batch ya mwanzo 2005. Baada ya kuhitimu alichaguliwa kuwa Mhadhiri Msaidizi na mwaka mmoja baadae alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamili na kurejea MuM ambako amekuwa akifanya kazi mpaka mauti yalipomkuta.
Pia Al akhy Jaffar Siraj alikuwa ndio kiongozi wa umoja wa wanafunzi waliomaliza chuo kikuu cha waislam morogoro
Watu mbali mbali pamoja na uongozi wa radio imaan na chuo kikuu cha waislam wamemtakia mapumziko mema Al akhy Jaffar Siraji
Post by Radio Imaan.
Post by Athumani Chuji.
0 comments :
Post a Comment