REDIO IMAAN NA KWA NEEMA FM zafungiwa kwa miezi sita kisha mamlaka ya habari(TCRA) kupitia Makamu mwenyekiti wa maadili mh Walter Bgoya imeagiza vituo hivyo vya habari kukiri makosa na kuahidi kwamba hawatorudia.Pia kituo kingine cha habari kinachofahamika kama CLOUDS FM kimepewa onyo kali la kutorudia kosa lao pia kimetozwa faini ya sh milioni tano pamoja kuamuriwa kuondoa vipindi ambavyo viko kinyume na tasnia ya habari.
MAKOSA YA KUFUNGIWA KWAO.
KWA NEEMA FM
imefungiwa kwa kosa la kuhamasisha vurugu ambazo zilitokea huko Geita kuhusiana na maswala ya nani achinje kati ya waislam na wakristu.Hivyo TCRA kupitia makam mwenyekiti wamewapa KWA NEEMA FM adhabu ya miezi6 kutokuwepo hewani
.
REDIO IMAAN imefungiwa kwa kosa la kuhamasisha watu kutoshiriki sensa ya watu na makazi,zoezi ambalo lilifanyika mwaka jana 2012.Hivyo TCRA imeifungia RADIO IMAAN kwa miezi sita pamoja na kuandika barua ya kuahidi kutorudia kwa jambo hilo
.
CLOUDS FM imetozwa faini kwa kosa la kuendesha vipindi ambavyo vipo kinyume na maadili na kusemekana kwamba vipindi hivyo vinasapoti ushoga.Vipindi ni kile cha BREAK FAST ambacho ndani yake kuna kipindi cha JICHO LA NG'OMBE.Hivyo TCRA pamoja na adhabu ya kutozwa faini pia CLOUDS FM imeamriwa kuondoa kipindi na kutoweka kipindi mithili ya hicho.
RUFAA
Kwa mujibu wa Makamu mwenyekiti wa TCRA redio zote huru kukata rufaa dhidi ya adhabu hizo ambazo zimetolewa na mamlaka ya habari ndani kipindi cha siku 30 kutoka kutangazwa kwa adhabu hizo.
waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo wa kutangazwa kwa adhabu hizo
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment