-->

HASARA YA SHILINGI BILIONI 1.3 YAJITOKEZA NCHINI


TEMBO, simba, chui, fisi na nungunungu kutoka Hifadhi ya Taifa ya Wanyama ya Serengeti wamesababisha hasara inayofikia Sh bilioni 1.3 kwa kuvamia makazi ya wananchi na kuharibu ekari zipatazo 6,000 za mashamba, kujeruhi na kuua mifugo. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira wilayani Serengeti, Michael Kunani, alisema hiyo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa matukio ya wanyama hao uliofanyika kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi 2016. 

Alisema uchunguizi huo umebaini kuwapo na uharibifu wa mazao, mauaji ya mifugo ambako wastani wa watu watatu huuawa kila mwaka katika vijiji vya Robanda, Singisi,Makundusi na Nyamatoke. 

Matukio hayo hutokea wanyama hao wanapofika katika makazi ya wananchi na baadhi ya watu wanapokwenda kufanya ujangili katika maeneo ya uhifadhi, alisema. 

“Mwingiliano huo wa binadamu na wanyamapori umesababisha kubadilika kwa tabia za wanyama hao kama tembo kwenda na kubomoa nyumba na kuangusha vihenge vinavyohifadhi nafaka hivyo kuongeza hasira kwa wananchi.

CHANZO:MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment