-->

4U MOVEMENT TANZANIA WATOA UFAFANUZI DHIDI YA HALI YA LOWASA KWA SASA

HABARI 4U MOVEMENT TANZANIA.  
Edward Ngoyai LowassaTunayo furaha kuwapongeza kwa uvumilivu na UMOJA wetu tulio uonesha na tulionao hata sasa na kwa kipindi chote katika kumpambania Edward Lowassa Kupata tiketi ya Urais ndani ya chama cha mapinduzi. Malengo yetu Balozi wetu Edward Lowassa awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si Ukatibu au Uenyekiti wa chama kwani Malengo yetu ni ukombozi wa Maisha ya Watanzania wote. Tumesikitishwa na vikao vya Maamuzi ya Chama kwa kuto Mpitisha mtu anae kubalika nje na ndani ya chama kama alivyo sema Mwl. Julius Nyerere, 4u movement haiungi Mkono maamuzi hayo yaliogubikwa na Sintofahamu nyingi. Tunawaomba muwe watulivu na wenye subira kwani Mchakato wa Kidemokrasia wa kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado upo wazi kwa majibu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumaini letu ni Lowassa kwa sababu ndie Pekee tunaemuamini na Anauwezo. Alipo Edward Lowassa Tupo. Pia zipo Taarifa kuwa hayuko salama, hizo Taarifa si za kweli ni upotoshaji. Edward Lowassa yupo salama na anaendelea na majukumu yake. Tusubiri mpaka atakapo toa neno na sisi viongozi tutawajuza nini cha kufanya. Tutawapatia muongozo kila inavyo bidi. Ahsanteni

Mr Hemed Ally

Mratibu Taifa (National Coordinator)

@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO

IMEWEKWA MTANDAONI NA: Gabriel Gregory Ishole
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment